Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema ushirikiano baina ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais umechangia katika kudumisha Muungano na kuimarisha usimamizi endelevu wa mazingira.
Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kikao kazi cha Watumishi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.
Kutokana na hatua hiyo, Dkt. Jafo ameshukuru na kuwapongeza viongozi na watumishi kwa ujumla kusukuma mbele ajenda ya mazingira kupitia usimamizi wa kanuni na miongozi mbalimbali ya mazingira.
“Ndugu zangu watumishi nitoe pongezi za dhati kwenu kwani mmetumia vyema utaalamu wenu katika kusimamia vizuri hifadhi ya mazingira kupitia kampeni zetu mbalimbali za mazingira,“ amesisitiza.
Pia, Waziri Jafo amewahimzia wasimamizi wa miradi inayotekelezwa na Ofisi hiyo kuendelea kuisimamia vyema ili iendelee kueleta tija kwa wananchi katika maeneo yenye changamoto za mazingira.
Amewahimiza watumishi hao kuishi kwa kupendana na kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa kujituma ili kuacha alama nzuri.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amewahimiza watumishi wa ofisi hiyo kuwa wabunifu ili kupata matokeo makubwa katika utekelezaji wa majukumu.
Pamoja na kuwapongeza watumishi hao, pia amewataka waendelee kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwani kwa kufanya hivyo kutachangia katika kusukuma mbele maendeleo.
Pia, ametoa rai kwa watumishi kupitia ubunifu na taalama zao watumie fursa ya teknolojia inayopatikana ili kuboresha mazingra ya kazi na hivyo kufanya utendaji wa kazi kuwa wenye tija.
“Kama mnavyojua sasa hivi tumeshaanza mwaka mpya wa fedha na hivyo nina matarajio makubwa sana kutoka kwenu watumishi kuona mnafanya kazi kwa bidii na hivyo Ofisi inapata matokeo mazuri,” amesisitiza Katibu Mkuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Ofisi yake wakati akifungua kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.
Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao kazi cha watumishi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufungua kikao kazi jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (kushoto) akiagana Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...