Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WATU
wanne wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonganga uso
kwa uso na gari aina ya Scania katika Kijiji cha Mapatano, kata ya
Mbwewe Wilaya ya Kipolisi Chalinze.
Ajali
hiyo inaelezwa kwamba ilitokea saa nane na nusu usiku wa kuamkia agost 3
mwaka huu ambapo gari yenye namba za usajili T 104 CBU Toyota Prado
ikitokea Dar es Salam kwenda Same ikiendeshwa na Nechi Msuya aliyekuwa
Mkurugenzi wa benki ya
ABSA iligongana na Lori.
ABSA iligongana na Lori.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo alieleza kwamba gari hiyo
ikiendeshwa na Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa (45-50) iligongana na
gari yenye namba za usajili T 881 DWU/ T 888 DWU aina ya scania
ikiendeshwa na dereva Philipo Mtisi (43) ikitokea Arusha kwenda Dar es
Salaam.
Aliwataja
waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni dereva wa Toyota Prado Nechi
Msuya, Dayana Mageta, Nora Msuya ambaye alikuwa mwalimu wa Chuo Kikuu
cha Mzumbe tawi la Dar Es Salam na abiria mwingine wa kike anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 30-35 jina halijafahamika.
Kamanda
Lutumo alisema chanjo cha ajali hiyo ni dereva wa Toyota Prado kuhama
kutoka upande wa kushoto kwenda kulia kisha kugongana uso kwa uso na
Lori hilo.
Miili
ya waliofariki katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba
ikisubiri uchunguzi wa daktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.
Vilevile
alitoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara kuchukua tahadhari na
kuzingatia sheria za usalama kuepukana na qjali zinazoweza kusababishwa
na uzembe.
Hata
hivyo, madereva wa vyombo vya moto wetahadharishwa kutumia vileo
wanapoendesha vyombo vya moto kwani imekuwa chanzo cha kusababisha ajali
za barabarani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...