Bungeni - Dodoma

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent L. Bashungwa(Mb) amemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na ameahidi kudhibiti  na kupambana na Rushwa katika mikataba, manunuzi na usimamizi wa miradi.

Amesema hayo leo tarehe 06 Septemba 2023  Bugeni Dodoma wakati alipota nafasi ya kujibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge Kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Kuapishwa na kuwa Waziri wa Ujenzi.

“Ninamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini, Mimi pamoja na Niabu Waziri tunamhadi kufanya kazi kwa bidii kwa kupambana na kudhibiti Rushwa hasa kwenye maeneo ya mikataba, manunuzi na usimamizi wa miradi, ili dhamira ya Mheshimiwa Rais na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi uende Vyema”

Aidha, Wakati akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Mhe. Katani Ahmed aliyetaka kujua lini Serikali itatenga fedha ya dharura kujenga kipande cha Barabara ya Nguja - Mkwiti - Tandahimba yenye maeneo Korofi.

Bashungwa amewaigiza Maneneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mikoa yote kufanya Upembuzi yakinifu na kubaini maeneo yote korofi ya Barabara na kuyawasilisha Wizarani ili yaweze kupewa kipaumbele wakati wa kuandaa bajeti.

“Nitumie nafasi hii kuwaelekeza Mameneja wa TANROADS mikoa yote kuangalia maeneo yote korofi na kufanya Upembuzi yakinifu na kuyawasilisha Wiazarani ili yapewe kipaumbele wakati wa kuandaa bajeti” amesema Bashungwa

Kadhalika, Mbunge wa Tandahimba, Mhe. Katani Ahmed alitaka kujua Je, ni lini ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara kutoka Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala hadi Masasi utaanza, ambayo ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi 2020 na ahadi ya Mheshimiwa Rais.

Wakati akijibu swali hilo, Bashungwa amesema ujenzi wa barabara ya Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala – Masasi yenye urefu wa kilometa 210 unatekelezwa kwa awamu ambapo ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mtwara – Mnivata (km 50) umekamilika kwa kutumia fedha za ndani. 

Bashungwa amesema kuwa sehemu ya barabara ya Mnivata – Newala - Masasi (km 160) chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesainiwa tarehe 21 Juni, 2023 kwa sehemu za Mnivata – Mitesa (km 100) na Mitesa – Masasi (km 60) pamoja na ujenzi wa Daraja la Mwiti, kwa sasa Makandarasi wa sehemu zote mbili wapo katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...