Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Alpha Tanganyika Flavour Limited ya  mkoani Kigoma inayojishughulisha na biashara ya Samaki aina ya Migebuka imetoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika(AGRF) unafanyika nchini Tanzania.

Imesema wao kama Kampuni inayotambulika kimataifa wanashukuru kupata nafasi ya kushiriki mkutano huo na imekuwa fursa kwao kukutana na wadau mbalimhali waliohudhuria mkutano huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alpha Tanganyika Flavour Limited,  Alpha Nondo amesisitiza kwa kipekee wanampongeza Rais Samia kwa kufanikisha mkutano huo kufanyika nchini.

Amesema Dk.Samia anajua ili uwe kiongozi lazima uwe na elimu kwa sababu elimu ina nguvu na ndio maana amehakikisha  mkutano huo unakuja nchini akimiani mbali ya fursa Watanzania watajivunza na kubadilishana uzoefu na wadau wengine walioko katika jukwaa la mfumo wa chakula Afrika.

"Rais wetu anafanya hivi kwa manufaa ya watanzania na tunampongeza sana, lakini katika huu kuna faida nyingi kwani huduma zote ambazo zinahitajika kwa wageni wa mkutano huo zitafanywa na Watanzania.

" Wageni wanaingia na wanakula ,kunywa, kulala,wanalala hoteli za Tanzania na usafiri wanatimia wa Tanzania,  hivyo unaweza kuona umuhimu na fursa za mkutano huu."

Kuhusu kampuni yao amesema wanafanya biashara ya  samaki wa ziwa Tanganyika aina ya Migebuka na tunashukuru tumekuwa tukiuza samaki katika nchi mbalimbali zikiwemo za Ulaya...

" Na kwa kuwa tunafanya shughuli zetu katika viwango vya juu vya ubora imetuwezesha kuuza samaki mahali kokote duniani na bahati nzuri Migebuka inapatikana Ziwa Tanganyika peke yake"

Amesema katika Ziwa Tanganyila kuna aina nyingine za samaki lakini wao wameamua kujikita katika kuuza samaki aina ya Migebuka ambao wanawavua na kisha kuwaanda kwa maana ya kuwachaka na kukausha kwa mashine maalum na baada yapo wanaingiza sokoni.

"Tunauza Migebuka katika nchi mbalimbali na baadhi ya nchi hizo ni Marekani, Canada lakini pia tunafanya kazi na Umoja wa Ulaya kwasababu tunatambulika kimataifa na Kampuni yetu ndio pekee imekidhi vigezo vya kimataifa katika Ziwa Tanganyika."

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alpha Tanganyika Flavour Limited Alpha Nondo(kushoto) akiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika picha ya pamoja baada ya kuzungumza na  waandishi wa habari kwenye banda lake lililopo katika Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika( AGRF) unaoendelea jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alpha Tanganyika Flavour Limited Alpha Nondo akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye banda lake lililopo katika Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika( AGRF) unaoendelea jijini Dar es Salaam



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...