Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni ya mikopo ya nyumba inayotoa fursa kwa wananchi ya kupata mkopo kuanzia sh milioni 20 hadi bilioni 1 sambamba na uhuru wa kulipia mkopo huo kidogo kidogo kila mwezi katika kipindi cha hadi miaka 25. Hatua ya benki hiyo inatajwa kuwa inalenga kuchochea kasi ya upatikanaji wa makazi bora nchini.
Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo inayofahamika kama ‘Mkopo wa Nyumba wa NBC’ ilifanyika Jumatano jioni jijini Dar es Salaam ikihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mpango huo ikiwemo Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Kampuni ya Ujenzi ya CPS, kampuni ya usambazaji na uuzaji wa bidhaa za ujenzi ya Nabaki Afrika, baadhi ya viongozi wa serikali, wateja pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw Masuke alisema ujio wa kampeni hiyo siyo tu unawapa fursa Watanzania kununua nyumba, bali pia unalenga kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika jamii kupitia upatikanaji wa makazi ya uhakika sambamba na kukuza sekta ya ujenzi wa nyumba za biashara nchini.
“Ujenzi wa nyumba huleta ajira kwa watu mbalimbali, kutoka kwa wafanyakazi wa ujenzi hadi wachuuzi wa vifaa vya ujenzi. Pia, inachochea mzunguko wa pesa kupitia manunuzi ya vifaa vya ujenzi, na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi zinazopatikana kutokana na matumizi ya nishati za umeme na maji katika nyumba hizo, hivyo kampeni hii inafungua fursa kubwa zaidi ya kiuchumi kupitia mnyororo mzima wa sekta ya ujenzi,’’ alifafanua.
Bw Masuke aliitaja mikopo inayohusishwa kwenye mpango huo kuwa ni pamoja na mkopo wa kununua nyumba, mkopo wa kukamilisha au kukarabati nyumba pamoja na Mkopo wa dhamana ya nyumba.
“Kupitia mkopo wa kununua nyumba tunashirikiana na makampuni mbali mbali ikiwemo kampuni ya ujenzi ya CPS ambapo tunawezesha wateja kununua nyumba kwa riba nafuu kwa gharama ya sh milioni 20 hadi bilion1 kwa muda wa miaka 25 ambapo benki itatoa mkopo wa hadi asilimia 85 ya thamani ya nyumba.’’
‘’Kwa upande wa mkopo wa kukamilisha au kukarabati nyumba, NBC tunatoa fursa ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ambayo mteja ameanza ujenzi lakini kutokana na sababu mbalimbali ikatokea kwamba ameshindwa kumalizia ujenzi au ukarabati wa nyumba. Katika kipengele hiki pia tumeshirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo kampuni za vifaa vya ujenzi kama Nabaki Afrika ambapo mteja wa NBC atapata punguzo la bei katika manunuzi ya vifaa kutoka kwao.’’ Alitaja.
Akifafanua kuhusu Mkopo wa dhamana ya nyumba, Bw Masuke alisema benki hiyo inamuwezesha mteja kupata mkopo kwa kuweka nyumba yake kama dhamana, na anaweza kutumia fedha za mkopo huo kwa mambo mbalimbali kulingana na mipango yake ya kimaendeleo.
“Hii ni fursa nzuri sana ya kufanikisha malengo binafsi iwe ni kuwekeza kwenye biashara, kuweka akiba katika Hati Fungani, au kwenye miradi mingine ya maendeleo. Aidha kupitia mikopo hii tuna dhamana ya kuwapatia punguzo la bei kwenye ununuzi wa vifaa vya ujenzi kutoka Nabaki Afrika Ltd,’’ Alisema huku akibainisha kuwa mikopo hiyo pia inahusisha bima ya mali na bima ya Maisha ili kuhakikisha kuwa nyumba za wanufaika wa mkopo huo na familia zao zinakuwa salama wakati wote.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Fedha wa TMRC, Oswald Urassa alisema kwasasa kasi ya upatikanaji wa mikopo ya nyumba nchini bado ipo chini ya asilimia moja ikilinganishwa na baadhi ya mataifa jirani ikiwemo Kenya yenye asilimia 1.8 na Rwanda iliyofikia asilimia 4 huku akiipongeza benki ya NBC kwa kuja na huduma hiyo ambayo itachochea ongezeko la makazi bora hapa nchini.
“TMRC tumejipanga vema kuhakikisha kwamba tunashirikiana vema na NBC kufanikisha mpango huu muhimu unaoenda sambamba na adhma ya serikali ya kuboresha makazi ya wananchi wake. Mkopo huu unaweza kuvutia watu wengi zaidi hasa kwa kuzingatia kwamba hata muda wa merejesho yenyewe ya mkopo ni mrefu kufikia hadi miaka 25, kipindi ambacho kinamuwezesha mkopaji kufanya marejesho kwa kiasi kile kile au chini zaidi ya kiasi anacholipa kodi kwenye nyumba ya kupanga au ya kukodi. Niwasihii sana Watanzania wachangamkie fursa hii,’’ alisema.
Awali akizungumzia sababu zinazokwamisha kasi ya ujenzi wa nyumba nchini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya CPS inayosimamia ujenzi wa mradi wa nyumba wa Fumba uliopo Zanzibar, Bw Sebastian Dietzold aliitaja changamoto za kiuchumi miongoni mwa watanzania kama ya moja ya kikwazo kikubwa katika kufanikisha ujenzi wa makazi bora, huku akitaja ujio wa mkopo wa Nyumba wa NBC kuwa ni moja ya suluhisho muhimu katika kukabiliana na changamoto hiyo.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Nabaki Afrika Russel Stuart alisema kupitia mpango huo kampuni yake imejipanga kutoa punguzo la asilimia 5 hadi asilimia 15 kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi wa nyumba kwa wateja watakahusishwa na mkopo huo katika kipindi chote cha ujenzi wa nyumba zao.
Kampeni hiyo ya ‘Mkopo wa Nyumba wa NBC’ imekuja kipindi ambacho takwimu zinaonyesha kuna ongezeko la uhitaji wa nyumba 200,000 kila mwaka hapa nchini huku taifa likiwa linakibiliwa na upungufu wa nyumba za makazi milioni tatu kwasasa.
Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke (wanne kushoto) na Mkurugenza wa Fedha wa Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Oswald Urassa (wa tano kulia) wakishirikiana kuzungurusha nembo maalum yenye muonekano wa nyumba ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Mkopo wa Nyumba wa NBC’ inayolenga kuchochea kasi ya upatikanaji wa makazi bora nchini wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika siku ya Jumatano jijini Dar es Salaam. Wengine ni wadau wa kampeni hiyo akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya CPS Bw Sebastian Dietzold (wa tatu kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Nabaki Afrika Russel Stuart na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mikopo inayohusishwa kwenye mpango huo ni pamoja na mkopo wa kununua nyumba, mkopo wa kukamilisha au kukarabati nyumba pamoja na Mkopo wa dhamana ya nyumba.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw Masuke (pichani) alisema ujio wa kampeni hiyo siyo tu unawapa fursa Watanzania kununua nyumba, bali pia unalenga kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika jamii kupitia upatikanaji wa makazi ya uhakika sambamba na kukuza sekta ya ujenzi wa nyumba za biashara nchini.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Fedha wa TMRC, Oswald Urassa (pichani) alisema kwasasa kasi ya upatikanaji wa mikopo ya nyumba nchini bado ipo chini ya asilimia moja ikilinganishwa na baadhi ya mataifa jirani ikiwemo Kenya yenye asilimia 1.8 na Rwanda iliyofikia asilimia 4 huku akiipongeza benki ya NBC kwa kuja na huduma hiyo ambayo itachochea ongezeko la makazi bora hapa nchini.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Nabaki Afrika Russel Stuart (pichani) alisema kupitia mpango huo kampuni yake imejipanga kutoa punguzo la asilimia 5 hadi asilimia 15 kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi wa nyumba kwa wateja watakahusishwa na mkopo huo katika kipindi chote cha ujenzi wa nyumba zao.
Awali akizungumzia sababu zinazokwamisha kasi ya ujenzi wa nyumba nchini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya CPS inayosimamia ujenzi wa mradi wa nyumba wa Fumba uliopo Zanzibar, Bw Sebastian Dietzold (pichani) aliitaja changamoto za kiuchumi miongoni mwa watanzania kama ya moja ya kikwazo kikubwa katika kufanikisha ujenzi wa makazi bora, huku akitaja ujio wa mkopo wa Nyumba wa NBC kuwa ni moja ya suluhisho muhimu katika kukabiliana na changamoto hiyo.
Hafla ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mpango huo ikiwemo Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Kampuni ya Ujenzi ya CPS, kampuni ya usambazaji na uuzaji wa bidhaa za ujenzi ya Nabaki Afrika, baadhi ya viongozi wa serikali, wateja pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi.
Home
HABARI
Benki ya NBC Yazindua Kampeni ya Mkopo wa Nyumba, Kuchochea Kasi Upatikanaji Makazi Bora.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...