Hiyo ni Kauli ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Chiriku Hamis Chilumba kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwake kwenye kikao Cha baraza la madiwani la hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliofika kufuatilia sakata la hivi karibuni kuhusu kukataliwa kwake na baraza la madiwani pamoja na kusimamishwa kazi watumishi wake watatu.
Chilumba alisema Toka kutokea Kwa sakata Hilo anapigiwa simu nyingi Sana na waandishi wa habari licha ya wengine kuja moja Kwa moja ofisini kwake wakitaka azungumzie sakata Hilo, nawaambia "Tuiachie tume ya uchunguzi" ,alisema Chilumba.
Aidha Chilumba alidai yeye ndiye aliyetuhumiwa hivyo kama yeye ametuhumiwa mamlaka itakayochunguza tuhuma hizo ndiyo itabaini kuwa tuhuma hizo ni za ukweli au sio kweli ,kwake yeye anatakiwa kujibu tuhuma lakini sio kuingilia majukumu ya tume alifafanua Chilumba.
Baada ya majibu hayo waandishi wa habari hao akiwemo wa EATV ,Newton Yendayenda na Dita Nyoni wa Channel ten walishiriki zoezi la mheshimiwa mbunge Vitta Kawawa kikabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 17 katika zahanati ya Kijiji Cha Kilangalanga .
Wakati wa makabidhiano hayo waandishi wa habari hao walijawa na sintofahamu kuona diwani wa kata ya Luchili Othuman Njovu akimwaga sifa Kwa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Kwa msaada mkubwa alioupata katika kukamilisha zahanati ya Kijiji Cha Kilangalanga.
Waandishi wa Habari hao waliendelea kushuhudia wananchi akiwemo Said Mbawala aliyewahi kuwa diwani wa kata hiyo katika mahojiano na waadishi wa habari hao kuhusu kupata maoni yake kuhusu kukabidhiwa Kwa vifaa katika zahanati Yao ya Kijiji hicho hakusita kumshukuru mkurugenzi wa Halmashauri Kwa jitihada zake za kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika na inaanza Kutoa huduma na kuwaacha waandishi wa habari hao wakijadiliana kuwa mkurugenzi anayekataliwa na madiwani lakini wananchi wanamkubali walisema waandishi hao.
Baraza la madiwani la hivi karibuni limemkataa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamis Chilumba na kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa idara ya elimu ,afya na manunuzi huku wananchi wakiwamwagia sifa watumishi hao Kwa kazi nzuri wanazozifanya za kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo Yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...