ILI kuhakikisha sekta ya usafiri hasa ya usafiri wa bodaboda inatambulika vyema kwa jamii, Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (CMPD) kwa mara ya kwanza kimeshirikiana na kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali nchini Tanzania, Tigo, kampuni ya kubashiri michezo ya Betika, EFM, pamoja na Dk.Mwaka ForePlan International kuandaa Kuzindua mashindano ya mpira wa miguu unaofahamika kama “Tigo Pesa Bodaboda Cup 2023”.

Mashindano ya “Tigo Pesa Bodaboda Cup 2023” yanalenga kuwakutanisha madereva wote wa bodaboda ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kuwaelimisha kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta hii ya bodaboda ikiwemo malipo ya kidijitali, ulinzi na usalama barabarani kama sehemu ya mpango wa kupunguza umasikini miongoni mwa wananchama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Katibu wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam, Daud Laurian amesema; "Sekta ya bodaboda ina fursa nyingi za kiuchumi, hivyo ni muhimu kuwaunganisha na kuwaonyesha jinsi ya kuchangamkia na kunufaika na fursa hizi."

"Tasnia ya bodaboda inamchango muhimu sana hapa nchini, madereva wengi wa bodaboda ni watu wenye bidii wanaolenga kubadilisha maisha yao,Zaidi ya hayo, tasnia yetu ina fursa nyingi za kiuchumi, hivyo bodaboda hawezi kukosa rasilimali za kuboresha maisha yake." aliongeza Laurian.

Meneja wa Malipo ya Wafanyabiashara wa Tigo Pesa, Edgar Mapande, akiwa katika uzinduzi alisema, "Ushirikiano huu na CMPD una manufaa makubwa kiuchumi yatakayo saidia madereva wa bodaboda kutimiza baadhi ya malengo yao, ikiwa ni pamoja na kunufaika na faida za uchumi wa kidijitali kwa kutumia Lipa Kwa Simu ya Tigo Pesa kama suluhisho la kukusanya malipo. Kwa pamoja, tunaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa madereva wa bodaboda, familia zao na nchi kwa ujumla. Ushirikiano huu ni fursa kubwa kwa vijana hasa wakati huu tukifanya kazi kuelekea kuendeleza mfumo wa uchumi wa kidijitali kupitia “malipo madogo."

Mashindano ya Tigo Pesa Bodaboda Cup 2023 yatahusisha jumla ya timu 64 kutoka wilaya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam na semina mbalimbali zitatolewa maeneo ambayo mashindano haya yatafanyikia. Aidha, madereva wa bodaboda watapata fursa ya kujifunza faida za kutumia Lipa Kwa Simu kama njia ya kupokea malipo. Jumla ya viwanja vinne vya mpira wa miguu vitatumika kwa mashindano hayo, ikiwa ni pamoja na uwanja wa Machava Kigamboni, Uhuru wa Temeke, Ukombozi wa Ubungo na Airwing wa Ilala.

CMPD ni chama kinachosimamia madereva na wamiliki wa pikipiki katika Mkoa wa Dar es Salaam, kilianzishwa mwaka 2016, kinasaidia madereva wa bodaboda kupata mikopo ya pikipiki, viwanja, simu, leseni za udereva pamoja na bima ya afya kupitia taasisi za kifedha nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...