Na Jane Edward, Arusha
WAZIRI wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Moses Nnauye amesema Arusha inakuwa mwenyeji wa kuwa na jengo la Posta Afrika kwa mara ya kwanza ambapo mgeni Rasmi atakuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Nnape ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa kikao cha 41 cha baraza la utawala la umoja wa Posta Afrika (PAPU)kilicho wajumuisha viongozi na wadau wa Posta kwaajili ya kuandaa ajenda ya pamoja katika nchi hizo ambapo kikao cha baraza la posta Duniani kitafanyika Oktoba Mwaka huu.
Amesema jengo hilo litalichangamsha jiji la Arusha kutokana na ujenzi wake kuwa wakipekee na namna lilivyokaa ni kivutio tosha kwa utalii kwa kuzingatia Arusha ndyo kitovu cha utalii.
"Leo kulikuwa na kikao cha wasimamizi wa Posta Duniani ambapo wamekutana kujadiliana kuona namna wasimamizi wa huduma za posta wataendelezaje shughuli za Posta Kidigitali"Alisema
Ameongeza kuwa uwepo wa jengo la Posta Afrika ni ndoto za Hayati baba wa Taifa Julius Nyerere ambapo lengo hilo limetimia na kwa uzito huo ndio maana Rais anakuja kufungua jengo hilo.
Macris Mbodo ni posta masta Mkuu shirika la posta Tanzania anasema Tanzania ni mjumbe wa Posta Duniani na wamejitahidi kama posta kuhakikisha huduma za kiposta zinakuwa na kuendelea kuhamasisha Watanzania kuagiza bidhaa mbalimbali kwa kutumia posta kwa kupakua App ya posta kiganjani.
Pia amesema kuwa wanajitahidi kuboresha huduma kidigitali ili kuendana na kasi ya dunia ya sasa na kukua katika soko la kimageuzi.
Waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Macris Mbodo ni Posta masta Mkuu shirika la Posta Tanzania akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...