Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MEYA wa Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam Abdallah Mtinika amewaomba wananchi wa manispaa hiyo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa juu wote ili wote tubaki kuwa katika Tanzania iliyosalama.
Akizungumza wilayani Temeke wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na mipango ya utekelezaji kwa mwaka 2023/2024, Mtinika amesisitiza Tanzania ni dira ya usalama na uimara wa nchi zote za maziwa makuu.
“Tanzania tumezungukwa nan chi nyingi na kwa uimara wa usalama ambao tunao nchi kwetu imekuwa ndio faraja ya nchi zote zinazotuzunguka na kuendelea na shughuli zao kibiashara, kidoplomasia ,kiusafirishaji na mambo mengine.
“Kwasababu tunafahamu Tanzania ni kama mlangoni kwa hiyo amani yetu ni jambo la msingi sana,hivyo wana Temeke na Watanzania kwa ujumla tunawajibu mkubwa wa kulinda amani, tunawajibu wa kulinda nchi zetu.”
Aidha amesema kuwa hata kwa vijana wanapolinganisha maendeleo yetu na nchi nyingine lazima wafahamu hazikuendelea kwa ghafla bali zimeanzishwa miaka mingi.
“Sisi nchi zetu bado changa lakini kwa maendeleo tuliyonayo hata nchi zilizoendelea katika miaka kama hiyo hawakuwa na spidi kubwa ya maendeleo kama tuliyonayo sasa , hivyo niwatoe wasiwasi nchi yetu inakwenda vizuri.
“Viongozi wetu wetu wanatuongoza vizuri na huku chini tunasimamia vizuri na mambo yanakwenda vizuri na Tanzania hii ya awamu ya sita yajayo yanafurahisha.
Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa uongozi wa Manispaa ya Temeke unaipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo sera mbalimbali zenye lengo la kuwapelekea wana Temeke maendeleo.
Home
HABARI
MEYA MANISPAA YA TEMEKE AWAOMBA WATANZANIA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA, ASIFU HALI YA AMANI NA USALAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...