
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu amempongeza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi kwa umahiri wake katika kujibu maswali bungeni.
Mhe. Zungu ametoa pongezi hizo Septemba mosi, 2023 bungeni baada ya Mhe.Katambi kujibu maswali ya wabunge kwa niaba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mhe. Katambi ameeleza jitihada za serikali za kuboresha sekta ya uvuvi ikiwamo Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) inatengeneza programu tumizi (mobile app) ambayo itawawezesha wavuvi kupata taarifa za maeneo ya uvuvi ambako samaki wanapatikana kwa wingi. Aidha, programu hiyo imekamilika kwa asilimia 90.
Awali, Naibu Waziri Katambi alijibu maswali ya msingi na nyongeza yaliyoulizwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kubainisha hadi sasa wastaafu wote wa serikali wameboreshewa pensheni zao za kila mwezi.
Baada ya kujibu maswali ya wabunge, Mhe. Naibu Spika amesema “Mhe.Waziri nikupongeze kwa kucheza namba zote leo.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...