Mahakama ya Tanzania itakuwa mwenyeji Kusini mwa Awa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika utakaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 23 hadi 27 Oktoba, 2023.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Mhe, Ignas Kitusi alipokuwa anaongea na Wahariri na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) utafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,” Mhe Kitusi, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania amesema.
Amesema Mkutano huo utahudhuriwa na Majaji Wakuu 16 kutoka Angola, Botswana, Eswatin, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Tanzania Bara, Tanzania Visiwani (Zanzibar), Uganda, Zambia na Zimbamwe.
Wadau hao wanaotegemewa ni Wizara ya Fedha, Wizara ya Biashara, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Kutakuwepo pia na Bodi ya Utalii (TTB), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mabenki, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), Shirika la Maendeleo la Taifa (TPDC) na wengine.
“Lengo la kuwaalika wadau hawa ni kuwaonyesha wageni wetu huduma mbalimbali zinazotolewa nchini na kuungana na Serikali kutangaza vivutio nchini ikiwemo kuunga mkono Filamu ya ‘Royal Tour,” Mhe. Kitusi amesema.
Amesema kuwa jukwaa hilo la Majaji Wakuu limekuwa likikutana kila mwaka katika moja ya Nchi mwanachama kwa lengo la kuelimishana na kubadilishana uzoefu wa utatuzi wa changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma ya utoaji wa haki kwa wananchi.
Mkutano huo wa Wahariri na Waandishi wa habari umehudhuriwa pia na Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Masuala ya Familia, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mhe. Martha Mpaze, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Elimu na Habari, Bw. Machumu Essaba na sehemu ya wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano huo.
Katika kutambua na kukuza jukumu muhimu la Mahakama ndani ya Kanda, Majaji Wakuu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika waliamua kuanzisha Jukwaa mwaka 2003 ili, pamoja na mambo mengine, kuzingatia Utawala wa Sheria, Demokrasia, Uhuru wa Mahakama na kukuza mawasiliano ya pamoja.
Amesema maono au mtazamo wa Jukwaa hilo ni kuwa na Mahakama iliyobadilika, iliyo huru, iliyounganishwa na yenye umoja ambayo inakuza utawala wa sheria, haki, demokrasia na utawala bora ili kuhakikisha ustawi, usawa, amani na usalama wa raia wote.
Kanuni zinazoongoza utendaji kazi na uendeshaji wa umoja huo ni kukuza utawala wa sheria, utoaji wa haki bora inayopatikana kwa wote, utawala bora na maadili ya pamoja, uwazi, uhuru, kutopendelea, uadilifu na uwajibikaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Ignas Kitusi akisisitiza jambo alipokuwa anaongea na Wahariri na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahariri walioshiriki mkutano wa mahakama kuhusiana na Mkutaano wa Jukwaa la Majajibu utaofanyika nchini.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Balile akizungumza kuhusiana na umhimu wa vyombo vya habari katika mkutano huo jukwaa la majaji wa nchi zilizo Kusini mwa Afrika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...