Na Mwandishi Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Taasisi ya Mama  Ongea na mwanao 2021 chini ya Mwenyekiti wake Steven Mengele maarufu Steve Nyerere kupitia kampeni yao ya SAMIA NIVISHE VIATU kwa namna inavyoisaidia jamii katika mambo mbalimbali.

Ametoa pongezi hizo leo Septemba 19, 2023 wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika  Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo Stive Nyerere amesema kampeni ya SAMIA NIVISHE VIATU imeanza rasmi katika kijiji cha Namienje wilayani Luangwa kwa kuwavisha  viatu 200 watoto wa Kijiji hicho.

Amesema Kampeni hiyo ndio imeanza Katika mkoa huo wa Lindi,lakini itakwenda katika Wilaya zake na baadae itahamia Mtwara na Ruvuma, lengo likiwa kufika mikoa yote nchini

Amesema taasisi yake imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kampeni hiyo,lengo likiwa ni ' kusapoti' juhudi za  Serikali na Rais Samia kwa ujumla.

"Kampeni hii tutalifanya nchi nzima tumelenga vijijini na tutalifanya wenyewe na si kukabidhi kwa uongozi wa shule kwani  lengo letu kuhakikisha vinamfikia mlengwa" amesema Steve. 

Aidha  ameongezea kuwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuweka miundombinu mizuri katika sekta ya elimu hivyo wanawajibu kama taasisi inayounga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia kuhakikisha watoto wanaipenda shule.

Kampeni hiyo ilianza mwaka jana ambapo waligawa zàidi ya viatu 2000 kwa watoto katika mkoa ya pwani wilaya ya Kibiti na mkoa wa Tabora na wilaya zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...