Afisa Mawasiliano wa TGNP, Monica John, Akizungumza leo Septemba 2, 2023 jijni Dar es Salaam, katika maandalizi ya Tamasha  la 15 la Kijiinsia ambalo litafanyika  Novemba 7-10, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Viwanja vta TGNP.
Mratibu wa tamasha la jinsia la TGNP, Rose Mwalongo akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Deogratius Temba akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya waandishi wa habari wakichangia mada katika maandalizi ya Tamasha la Kijnsa litakalofanyika Novemba 7-10, 2023 Jijini Dar es Salaam.


Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MTANDAO wa kijinsia Tanzania (TGNP), kuadhimisha tamasha la 15 la kijinsia nchini kuanzia Novemba 7-10, 2023 jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mtandao huo.

Akizungumza leo Septemba 2, 2023 jijni Dar es Salaam, katika maandalizi ya tamasha hilo, Afisa Mawasiliano wa TGNP, Monica John, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Lilian Liundi  amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuliwa na watu zaidi ya 1500 ambao watatoka nchi mbalimbali wa hapa nchini na kutoka nje ya nchi.

"Tamasha hili litakusanya watu kutoka bara la Afrika na mabara mengine."

Amesema kuwa lengo la tamasha hilo kujifunza pamoja na kusheherekea mafanikio katika harakati za ukombozi wa mwanamke duniani na Tanzania kwa ujumla.

Pia tamasha hilo litaangalia changamoto zilizojitokeza ndani ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TGNP mwaka 1993 hapa nchini na kuangalia namna ambayo zitatatuliwa.

"Dhima ya tamasha hilo ni miaka 30 ya TGNP na TAPO la ukombozi wa mwanamke. Dhima hiyo inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa TGNP.

Katika tamasha hilo pia kutakuwa na mada mbalimbali zitakazo tolewa, watu watatoa uzoefu wao walivyofanikiwa ikiwa pamoja na kukutanisha watu mbalimbali wa vituo vya maarifa na taarifa kutoka kila mkoa.

Akizungumzia kuhusiana na namna ya kushiriki tamasha hilo, Monica amesema kuwa dirisha la kujisajiri litafunguliwa hivi karibuni ingawa tayari mialiko imeshatolewa kwa baadhi ya watu mbalimbali kutengemea na wanakotoka.

Monica ameeleza kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti kwani watakuwa wanasheherekea miaka 30 ya TGNP na kuadhimisha TAPO la Ukombozi wa mwanamke Tanzania, pia katika tamasha hilo wataangalia marekebisho ya sera na sheria zilizofanyiwa marekebisho tangu kuanzishwa wa TGNP hapa nchini.

Pia tamasha hilo litaangazia changamoto ambazo bado zinakwamisha Tanzania kutokuwa na usawa wa kijinsia na namna ya kutatua changamoto hizo.

Kwa upande wa Mwanaharakati Abas Ndelu, amesema kuwa kupitia TGNP ameweza kuhudhuria matamasha matano. Kwa mwaka huu amesema litakuwa tofauti kwani ni muunganiko wa maadhimisho ya miaka 30 ya mtandao huo tangu.

Amesema kuwa amepata manufaa makubwa ya kujitambua, kujua haki mbalimbali za binadamu, haki za wanawake pamoja na kujua sheria mbalimbali hivyo miaka 30 ya TGNP inamafanikio mengi kwao wenyewe pamoja na makundi mbalimbali.

Akizungumzia na mafanikio ya TGNP tangu kuanzishwa kwake, Taraka Seif, maarufu eneo la mabibo Taraka Nyange amesema kuwa Mtandao huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani yeye amepata elimu kutoka katika mtandao huo huku akijizolea umaarufu katika mitaa mbalimbali ya mabibo kwa kutetea haki za wanawake na watoto.

"Imefika mahali inapotokea mama au baba au mtu yeyote anamfanyia ukatili mtoto au mwanamke jamii inasema "Tutaenda kumwambia mama Taraka Nyange" hilo linanipa ujasiri sana wa kuendelea kupambana na ukatili katika mtaa wangu." Amesema Taraka

Kwa upande wa mwanaharakati aliyejiunga na TGNP tangu 2014, Mama Kunambi amesema kuwa TGNP imemtoa uoga kwani mwanzo alikuwa hathubutu hata kumkemea ndugu yake akifanya ukatili, lakini kwa sasa anaweza kwenda mahali popote kwenda kuripoti ukatili unapotokea.

Amesema kuwa mtaani kwake jamii inaogopa kufanya ukatili kutokana na yeye kuwepo katika mahali hapo. Amesema kwa upande wake Mafanikio Makubwa ya TGNP kwa miaka 30 ni kuwatoa woga wananchi ili waweze kugombea nafasi za uongozi na kushauri kuhusiana na bajeti yenye mrengo wa kijinsia kuanzia ngazi ya kifamilia kutokana na kila mwanafamilia kuwa na mahitaji yake.

"Kuelekea miaka 30 ijayo TGNP naomba izidi kupaza sauti ifike mpaka vijijini ili kila mmoja apate uelewa wa mambo ya kijinsia ili kusiwepo mtu ambaye atakatiliwa hata kwa bahati mbaya." Ameeleza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...