WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwasasa yamekuwa tishio kwa jamii yetu.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 2, 2023) baada ya kushiriki mbio hizo za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam ambapo ameisisitiza jamii ishiriki katika ulinzi wa watoto wenye ulemavu kwa kutoa taarifa kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya watoto hao.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaunga mkono wadau wa sekta binafsi katika jitihada zote za kuimarisha ustawi wa watoto wa Tanzania.

Aidha amesema kuwa Serikali kwa upande wake imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwa na ustawi na afya ya mtoto sambamba na kuimarisha upatikanaji wa huduma za elimu kwa watoto wenye ulemavu hapa nchini.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imehakikisha hospitali zote za wilaya zinatoa huduma za watoto wachanga ikiwemo huduma ya mama kangaruu (Mother Kangaroo) kwenye vituo vya afya nchini. “Hii ni huduma maalum ya kutunza watoto njiti na wale waliozaliwa na uzito mdogo”

“Serikali inatekeleza utoaji wa huduma ya kumsaidia mtoto mwenye usonji ili aweze kuongea (speech therapy) pia kutoa huduma ya kumsaidia mtoto ili aweze kufanya matendo mbalimbali (occupational therapy)”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka waandaaji wa mbio hizo waone namna bora ya kufikisha taarifa kwa umma kuhusu matunda ya mbio hizo ili jamii iweze kuhamasika na kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio za hisani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo, Dkt. Ibrahim Mwangalaba amesema katika kusherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwa benki hiyo waliamua kuandaa mbizo za hisani kwa lengo la kutafuta shilingi milioni 200 kusaidia vituo viwili vyenye uhitaji maalumu.

“Lengo la Mbio hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kukarabati majengo ya kituo cha kulea watoto wenye ulemavu wa akili maarufu kama “Mtoni Maalum” cha Dar es Salaam kinachohudumia watoto wenye mtindio wa ubongo, Down Syndrome na Usonji na kununua vifaa vya kusaidia watoto njiti kwenye hospitali ya KCMC iliyopo Moshi, Kilimanjaro.”WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa,akizungumza baada ya kushiriki mbio hizo za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo zilizofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa medali ya kumaliza mbio za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo na Mkuu wa Kanisa la KKKT, kwenye viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Septemba 2, 2023. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Dokta Ibrahim Mwangalaba.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpatia zawadi ya fedha mshindi wa kwanza kilomita 21 wanawake, Neema Kisuda, kwenye mbio za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo na Mkuu wa Kanisa la KKKT, kwenye viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es SalaamWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpatia zawadi ya fedha mshindi wa kwanza kilomita 21 wanaume, Michael Kishimba, kwenye mbio za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo na Mkuu wa Kanisa la KKKT, kwenye viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo baada ya kumaliza mbio za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo na Mkuu wa Kanisa la KKKT, kwenye viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mbio za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo na Mkuu wa Kanisa la KKKT, kwenye viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es SalaamWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa,akizungumza baada ya kushiriki mbio hizo za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo zilizofanyika leo Septemba 2,2023 katika viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...