Benki ya Mwanga Hakika imezindua kituo cha mafunzo kijulikanacho kama Mwanga Hakika Bank Training Academy kwa lengo kuongeza uelewa kwa vijana katika sekta ya benki na fedha nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Bw. Raymond Tarimo alisema kituo hicho kitakuwa msaada mkubwa katika kujenga uwezo wa vijana kwenye sekta ya fedha nchini.

“Tunaibua vipaji vya vijana na kuwajenga vijana wanatoka shule ili wawe na uwezo wa kuelewa sekta ya benki kuanzia mwanzo.

Ni imani yetu kwamba kituo hichi kitaleta tija kwa kuongeza ubunifu wa huduma tunazitoa kwa wateja wetu hapa nchini,” alisema.

Kituo hicho ni mahususi kwaajili ya wafanyakazi wa benki hiyo na wale ambao wanatarajia kuwa wafanyakazi wa benki hiyo ambapo kitatoa mafunzo juu ya uendeshaji na usimamizi wa masuala ya fedha ili kuongeza ufanisi wa huduma.

Programu zitakazotolewa zitahakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao kuendana na mahitaji ya soko nchini na kuwafikia wateja wa benki hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...