Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Jumamosi, Oktoba 14, 2023 amefanya Ziara ya kuwatembelea, kuwafariji na kuwajulia-hali watu mbalimbali huko Wilaya Ndogo Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Watu hao wote kutoka Mitaa ya Tumbatu Jongoe, ya Kigunda, Kusini, Lisani na Vuga, ni pamoja na Bi. Asha Khamis Haji, Bi. Sida Mwadini Khamis, Bi. Kazija Makame Makame, Bw. Ame Ame Bakar, Bw. Saleh Ali Saleh, Bi. Miza Haji Sheha, Bw. Suleiman Zubeir Abass, na Bi. Mnyasa Makame Mwadini.

Mheshimiwa Othman amefanikisha hatua hiyo akiendelea na Ziara yake ya Siku Mbili kisiwani Tumbatu, ambapo baadaye leo atajumuika na Wananchi na Waumini mbalimbali wa Kiislamu katika Hafla ya Maulid Makubwa, huko Mtaa wa Kichangani.

Kiitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Jumamosi, Oktoba 14, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...