VONGOZI wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Pwani COREFA, umeanzisha bonanza la soka la wanawake kuanzia ngazi ya shule za Sekondari lengo ikiwa  ni kuibua na kuviendeleza vipaji vya mabinti ambao watasaidiwa kutimiza  ndoto zao.  

Mwenyekiti wa Chama hicho, Robert Munisi, ameyasema hayo hivi karibuni wakati akiongea na Mabinti  wa shule mbalimbali za mkoa wa Pwani ambazo zimeshiriki bonanza hilo kwenye uwanja wa Maliasili uliopo Halmshauri ya Mji wa Kibaha.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vya mkoa huo ni kuinua soka la wanawake na katika  kufanikisha hilo   wanaandaa mabonanza ambayo yatawakutanisha ili kubadilishana uzoefu.

“Tuna mabinti wengi ambao wana vipaji vya kusakata kabumbu lakini kutokana na mazingira wanashindwa kuvionesha sasa COREFA tumeanzisha bonanza kwa ajili yao ambalo litakuwa endelevu itashiriki ili tuone uwezo wao na namna ya kuwasaidia,” amesema Munisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Soka la Wanawake mkoani humo, Mariam Songoro, alisema mpira ni ajira na kwa sasa wanawake wana nafasi kubwa ya kupata fursa ndani na nje ya nchi.

Alisema soka ni ajira kama zilivyoajira nyingine ambazo zikiinua maisha ya watu hivyo wanatoa nafasi kwa mabinti hao kuonyesha uwezo wao.

“ Huu ni mwanzo tu mabinti zangu bonanza hili litawanufaisha sana, kazi yenu kubwa ni kujituma uwanjani, kufanya mazoezi, nidhamu ambayo itawafikisha kule mnapopataka lakini msisahau kusoma kwa bidii ili muwe na uwezo wa kuongea lugha mbalimbali mtakapoenda kwenye nchi za wenzenu kucheza soka,"alisema.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...