Katika kusherekea miaka 60 ya ushirikiano kati ya Nchi Sweden na Tanzania kumetaajwa kuwa na mafanikio makubwa katika kutokomeza umasikini nchini tanzania kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, kutetea haki za wanawake na watoto pamoja na kuchangia uhuru wa ujieleza kupitia vyombo vya habari hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Afisa miradi, asasi za kiraia, habari na elimu ubalozi wa Sweden nchini Tanaznia Stephen chimalo wakati Balozi huyo akiwa mkoani Morogoro kutembelea na kujionea namna asasi za kiraia wanazifadhili zinavyofanya kazi.
Akizungumzia namna nchi ya Sweden inavyosaidia sekta ya habari pamoja na uhuru wa kujieleza hapa nchini mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani morogoro Nickson Mkilanya amesema Sweeden imekuwa ikifadhili miradi migi kwenye sekta ya habari hasa inayowahusu wanahabari moja kwa moja.
kwa upande wake afisa mawasiliano na utawala kutoka shirika lisilo la kiserikali la msaada wa kisheria (Morogoro Paralegal Center) Peter Kimath amesema shurika hilo limejipanga kuwasaidia wanaume wanafanyiwa vitendo vya ukatili kupitia ushirikiano wake na nchi ya Sweden
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...