Na Janeth Raphael - Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Utafiti wa kina wa Miamba ufanyike, kubaini maeneo yenye Madini na yapo kwa kiwango gani ili kuwawezesha wachimbaji kuchimba kwa uhakika na sio kwa kubahatisha.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo Leo Oktoba 21,2023 Jijini Dodoma wakati wa halfa ya uzinduzi wa mitambo mitano ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo na mitambo ya STAMICO kauli mbiu katika uzinduzi ni Madini ni maisha na utajiri.

"Utafiti ukafanyike ili kugundua maeneo yenye Madini na kuepukana na tabia ya kuchimbachimba bila kuwa na uhakika na kuepukana na tabia ya kuchimba Kwa kubahatisha ili Kila mmoja akapate tija katika sekta hii ya Madini na Taifa pia litapata mapato,"amesema Dkt.Samia

Pia Dkt.Samia amewataka wachimbaji nchini kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo nikuliibia taifa huku akidai huo si uzalendo.

“Tabia ya utoroshaji wa madini sio nzuri nawasihi kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini kama ni wazalendo msinge waza kutorosha madini sababu ndani tunaviwanda vya kutosha,tupeleke viwandani madini yakasafishwe yaongezewe thamani ili tupate fedha nyingi,”amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine Rais samia amewaagiza watendaji wa serikali kuyafanyia kazi mapungufu yanayotolewa na wafanyabiashara wa madini pamoja na wachimbaji kwani sekta hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa fedha ambazo matumizi yake upelekwa kusaidia jamii katika huduma za maji ,kilimo,huduma za afya ,ujenzi wa barabara na huduma zingine za kijamii.

Kadhalika alilitaka shirika la STAMICO kutembelea eneo lenye chumvi Mkoa wa Singida na kusaidia katika uwekezaji wake.

“Watengeeni wanawake maeneo kwa ajili ya uchimbaji na biashara ya madini katika ziara yangu nilipoenda Singida nilikutana na wanawake ambao wanazalisha chumvi sasa STAMICO muende mkakae nao na kuwasaidia ,” amesema Rais Dkt. Samia.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amesema kuwa kazi kubwa iliyofanyika katika Wizara ya Madini inatokana na maelekezo ya serikali ya awamu ya 6 hivyo alimtaka Waziri wa Madini kuyafanyia kazi maelekezo anayopewa na Rais ili kuwasaidia wachimbaji wadogo.

"Nataka kusema kuwa salama yako Waziri wa Madini ni kusikiliza na kutekeleza maelezo ya Rais nikuambie tu haya mazuri unayoyaona hapa leo katika Wizara ya madini ni malekezo ya Rais wetu,

Na kuongeza kuwa "Kiu ya mama yetu ni kuona wachimbaji wadogo wanaendelea kukua,Rais Samia anataka utulivu katika madini sasa basi niwatake viongozi wote mlipo hapa,Mawaziri,Manaibu Waziri na viongozi wote wa Serikali kuyachukua anayoyaongea Dkt.Samia hapa na mkayafanyie kazi,"alisisitiza Naibu Waziri Mkuu.

Naye Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema ili sekta ya Madini ipeleke mchango mkubwa Serikali ni lazima utafiti wa kina ufanyike kwaajili ya kuboresha kanzi data ya miamba.

"Tunapofanya utafiti wa kina kwaajili ya kuboresha kanzi data ya miamba itatusaidia kutanua wigo wa kutambua aina ya madini tuliyonayo na uwezo wa kuyachimba,"amesema Mavunde.

Amesema nchi imegawanywa katika vipande ambavyo vinatengeneza kilometra za miraba na hiyo ndio itatoa taarifa za msingi na za awali kuhusu madini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amebainisha kuwa kwa mwaka 2023 shirika limetenga faida ya Tsh. Bilion 17.3 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na vitendea kazi ambao thamani ya mitambo iliyozinduliwa leo imegharimu Tsh. Bilion 9.3.

“Shirika kwa miaka mitatu iliyopita lilikuwa na hali mbaya nalilikuwa linakusanya tsh. Bilion 1.3 na kwa sasa shirika linakusanya Tsh. Bilion 63.8 haya ni mafanikio makubwa, "alisema Dkt. Mwasse.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoka kukagua Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde mara baada ya kuzindua Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo pamoja na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde kuhusu Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo pamoja na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa Ufunguo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse kwa ajili ya kuwakabidhi Wachimbaji wadogo Mitambo ya Uchorongaji kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde kuhusu Mitambo ya kupasua na kusaga mawe crasher kwa ajili ya Wachimbaji wadogo kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa Ufunguo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse kwa ajili ya kuwakabidhi Wachimbaji wadogo Mitambo ya kupasua na kusagia mawe crasher kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Mkaa mbadala kwenye banda la Maonesho la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakati akipita kukagua shughuli mbalimbali za wachimbaji wadogo wa Madini kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda mbalimbali ya wachimbaji wadogo wa Madini kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vitu vya thamani kutoka kwenye banda mojawapo la wachimbaji wadogo Wanawake (WIMO) kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Shamrashamra katika uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...