Na. Jeshi la Polisi, Dar es Salaam, Oktoba 21, 2023

Baadhi ya Askari Polisi waliotimiza miaka 30 katika utendaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi ‘Wadepo 1993’ leo Oktoba 21, 2023 wametembelea Hospitali ya Polisi Kilwa road na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 2.5.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa umoja wa Askari hao, ACP. Ally Wendo amesema fedha hizo zimetokana na michango yao ambayo wamechanga na kununua vitu mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaopata huduma Hospitalini hapo.

“Tumeamua kufanya hivi kwa nia ya kumshukuru mungu kwa afya na uzima katika kipindi chote cha miaka 30 ya utendaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi kwa maana kuna baadhi ya wenzetu ambao tulitamani kuwa nao likini hatuponao kwa sababu mbalimbili”. Msaada uliotolewa ni pamoja na mashuka, Madawa mbalimbali, mito ya kulalia, sabuni za kufuli na katoni za maji ya kunywa.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, ACP. Dkt. Hussen Yahaya amewapongeza askari hao kwa kuwa na umoja ambao wameamua kutoa msaada katika Polisi ya Kilwa road “kwa kufanya hivi mtakuwa mmejisaidia nyinyi wenyewe, famila zetu pamoja na wananchi ambao wanapata huduma katika hospotali hiyo yenye hadhi ya rufaa ya Mkoa.


Katika hatua nyingine Dkt. Yahaya amesema hospitali hiyo ipo katika ujenzi wa jengo la hospitali la ghorofa tatu ambapo ametoa wito kwa vikundi kama hivyo, taasisi na asasi za kiraia katika kusaidia katika ujenzi na vifaa Hopitali hiyo ya Polisi ili iweza kutoa huduma zaidi za matibabu kwa wananchi.

1.      Mwenyekiti wa umoja wa wiliotimiza miaka 30 ‘Wadepo 1993’ ya utedaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi akimkabidhi boksi lenye Dawa mbalimbali Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, ACP. Dkt. Hussen Yahaya leo Oktoba 21, 2023 katika hafla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika Hospitali ya Polisi kilwa Road.

1.      Baadhi ya askari walio timiza miaka 30 ‘Wadepo 1993’ ya utedaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, ACP. Dkt. Hussen Yahaya leo Oktoba 21, 2023 katika hafla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika Hospitali ya Polisi kilwa Road.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...