Tasisi  ya Elimu Tanzania(TET) leo  tarehe 13/10/2023  imewasilisha mapendekezo  ya muundo wa elimu na mabadiliko yaliyopo kwenye Rasimu  ya mitaala  mipya ya elimu  kwa bodi na menejimenti  ya  Elimu  na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). 

Wasilisho hilo limefanyika  katika chuo cha Utalii cha VETA jijini Arusha. 

Lengo na wasilisho hili ni kuwapatia ufahamu Bodi na Menejimenti ya VETA kuhusu utekelezaji wa elimu ya Amali kwa Sekondari Hatua ya Chini ambapo utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa utafanywa na kusimamiwa na VETA

Mkurugenzi  Mkuu wa  Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt. Aneth Komba  amefanya wasilisho hilo mbele ya  mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Sifuni Mchome na wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti ya VETA ambapo ameeleza kuwa  mitaala mipya itasaidia  katika kumuandaa mwanafunzi kujitegemea kwani atakuwa na uwezo mzuri kutokana na ujuzi atakaopata kupitia mabadiliko hayo ya elimu.

"Maboresho haya ya Mitaala mipya ya elimu yamefanyika  kwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri  ya  Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha elimu itakayomuwezesha muhitimu  kuweza  kujiajiri na kuajiriwa baada ya kumaliza  masomo yake "amesema Dkt.Komba.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya  VETA, Prof Mchome ameeleza kuwa  wasilisho la Mitaala ni jambo jema kwao kuweza kupata uelewa kwa wajumbe na menejimenti nzima ya VETA na kuwa  itawazesha kujipanga katika  utoaji elimu kwenye eneo lao la Elimu ya Amali.

"Matarajio kwa wananchi ni makubwa kwenye maboresho ya mitaala hii hivyo ni wazi kuwa sasa kazi itaanza vyema ya kuhakikisha elimu imeboreshwa na kwamba sasa tunapaswa kujipanga vyema kama VETA alisema Prof. Mchome.

Katika hatua nyingine ,Dkt.Komba aliweza kukabidhi taarifa mbalimbali zilizofanyiwa kazi  kwa VETA kupitia nakala laini (soft copy) zitakazosaidia  katika utekelezaji wa rasimu ya mitaala .

Pia, katika kikao hicho, wajumbe wa bodi  na Menejimenti ya VETA, wameipongeza sana WyEST na TET kwa kazi kubwa ya maboresho ya Mitaala na kuahidi kusimamia utekelezaji na kutekeleza kwa umahiri katika eneo lao la Amali







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...