Na Mwandishi wetu - Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk.Venance Mwasse amewataka viongozi wanawake walioko katika sekta ya madini nchini kujiamini na kujitambua na wasiingie kwenye mitego mibaya.
Akizungumza leo Oktoba 18, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wanawake katika sekta ya madini, Dk.Mwasse pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha viongozi hao kujiamini na kuweka mipango inayowezesha taasisi wanazoziongoza kuwa na manufaa
"Unapochaguliwa au kuteuliwa kuwa kiongozi hakikisha unaweka mipango na kufanya maamuzi kwani kama kiongozi unashindwa kuwa na maamuzi wakati kuna watu nyuma yako hiyo itakuwa shida.Wanaoongozwa wanaamini kiongozi wetu anaweza kuamua kwa niaba yetu."
Hivyo Dk.Mwasse amesisitiza kwa kuwataka viongozi kuamua na kuwa na mipango ya kupeleka taasisi zao mbele na maamuzi hayo yawe yanawanufaisha wote huku akishauri wanaoongozwa wasiwakwaze viongozi wao huku akieleza ni vema kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu wataendelea kuwasaidia kwa kuwapa motisha.
Aidha Dkt Mwasse amesema Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Imeagiza mitambo kumi na tano (15) kwa ajili ya wachimbaji wadogo. na mitambo 10 imeshawasili Nchini na itazinduliwa na Rais Samia atawakabidhi tatehe 21, October 2023 siku ya jumamosi Jijini Dodoma
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...