Mgeni Rasmi Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile (kushoto) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu yenye lengo la kusaidia serikali katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG 2030). Viwango hivyo ni Uwazi katika kuripoti maendeleo endelevu (IFRS S1) na Uwazi katika kuripoti athari za kwenye mazingira (IFRS S2) vitakavyotumiwa na Taasisi zote nchini Tanzania za Umma na Binafsi kuanzia Januari 01, 2024. 
Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius A. Maneno.
Msaidizi Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu yenye lengo la kusaidia serikali katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG 2030) uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akziungumza kuhusu namna walivyojipanga kuweza kusimamia Viwango Vipya vya Hesabu vya kimataifa vya Kuripoti Maendeleo Endelevu na jinsi NBAA itakavyosaidia Taasisi mbalimbali katika kufikia malengo hasa kwenye kutumia viwango hivyo.
Mjumbe wa Bodi ya Kimataifa ya mahesabu kwa Sekta ya Umma(IPSASB), CPA Dkt Neema Kiure akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali waloudhuria uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu.
Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Witness Shilekirwa akitoa neno la shukrani kwa  Mgeni Rasmi Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile  pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Viwango vya kimataifa vya Maendeleo Endelevu.
Baadhi ya wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Bodi wakiwa kwenye uzinduzi wa Viwango vya kimataifa vya Maendeleo Endelevu uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Msaidizi Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno, Wafanyakazi wa Bodi hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Viwango vya kimataifa vya Maendeleo Endelevu uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...