Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amesema kuanza kutoa huduma kwa meli ya MV. Mbeya II kutarajiwa kurahisisha usafirishaji wa abiria na Mizigo kwa mikoa inayozunguka Ziwa nyasa.


Meli hiyo iliyokuwa imesimama kwa zaidi ya miezi sita kutokana na changamoto mbalimbali sasa imeanza rasmi kutoa huduma kupitia bandari ya Bandari ya Itungi Mkoani Mbeya na Bandari ya Mbambabay Mkoani Ruvuma.


Akizungumza wakati alipotembelea bandari ya Itungi Naibu Waziri Kihenzile amesema kuanza kutoa huduma kwa meli hiyo ni utekelezaji wa Sera ya Serikali ya kuhakikisha njia zote za usafiri zinaboreshwa ili kumpa nafasi mwananchi kutumia usafiri wowote anaoupenda kwa wakati anaotaka.


“Serikali ya awamu ya sita imeamua kuhakikisha njia zote za usafiri zinaboreshwa ndio maana mnaona kwenye majini meli hizi zinajengwa na kukarabatiwa, usafiri wa anga ndege zinanunuliwa, usafiri wa treni pia maboresho na ujenzi wa miundombinu unaendelea lengo ni kufanya mwananchi uchague kulingana na uwezo na muda wako’ amesema Naibu Waziri Kihenzile.


Naibu Waziri Kihenzile ameitaka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha changamoto zozote za meli hizo zinapojitokeza zinatatuliwa kwa wakati ili kutokwamisha shughuli za wananchi kwenye usafirishaji.


Kwa upande wake Mbunge wa Kyela Mhe. Ally Mlagila ameishukuru Serikali kwa kukamilisha ukarabati na kuanza kutoa huduma kwa meli hiyo kwani kutatatua changamoto ya usafiri hasa kwa maeneo ambayo bado miiundombinu ya barabra inaboreshwa.


Mmoja wa abiria wanaotumia usafiri huo Bw. Vitarisi Mkinga amesema Usafiri wa Meli hiyo umekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya kwani kwa sehemu kubwa hutumia usafiri huo kutoka eneo moja kwenda jingine.


Meli ya MV Mbeya ni miongoni mwa meli ambazo Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) iliikabidhi MSCL kwa ajili ya kuziendesha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...