Na Jane Edward, Arusha

Wiki ya azaki 2023 imefunguliwa leo rasmi jijini arusha na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta binafsi, na serikali Lengo ni kuwaunganisha wadau mbalimbali wakimaendele kutoka ndani na nje ya nchi ilikufikia maendeleo endelevu kwa kutumia teknolojia

Akizungumza mbele ya washiriki wa Mkutano wa Azaki uliowakutanisha wana Azaki iliyo fanyika jijini Arusha, Mrajisi wa asasi za kiraia wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ahmed Khalid Abdula amezitaka asasi za kiraia nchini kusaidia jamii katika kufikisha taarifa za matumizi sahihi ya teknolojia.

Amesema kuwa Matumizi ya teknolojia za kidigitali ikiwemo akili bandia ili waweze kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kupiga hatua maendeleo endelevu.

Akizungumzia lengo la Mkutano huo Mkurugenzi wa taasisi ya Foundation for Civil Society Fransis Kiwanga amesema ni kuwakutanisha wana Azaki pamoja kujadili masuala mbalimbali ya Azaki lakini kubwa ni kuangalia teknolojia itawasaidia vipi katika kurahisisha shughuli zao.

Amesema kuwa katika majadiliano yao watatoa fursa ya washiriki kuuliza na kujibiwa maswali kuhusu teknolojia ili waweze kufanya kazi kwa kuendana na soko la dunia ya sasa.

"Duniani kote Matumizi ya teknolojia yamechukua nafasi kubwa sana katika kurahisisha upatikanaji wa taarifa lakini kuhifadhi nyaraka mbalimbali na sisi kama wana Azaki tunaona ni wakati muafaka"Alisema


Kwa upande wake Balozi wa Uswis Didier Chasot amesema Uswis ikiwa ndyo wafadhili wakubwa wa Asasi hizo na wanazingatia kukuza ushiriki wa raia na uwajibikaji katika uendeshaji wa masuala ya Umma.


Aidha amesema CSR 2023 ichukuliwe kama jamii ya teknolojia kwa kuzingatia Dunia inaenda kasi sana katika Mapinduzi ya kiteknolojia na kidigitali.


Kwa upande wao washiriki Fatma Fungo afisa mtendaji Mkuu Zanzibar Maisha Bora Foundation anasema wiki ya azaki inazingatia katika masuala ya teknolojia ambapo akili bandia itasaidia wana Azaki katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutambua changamoto katika jamii na kupatia ufumbuzi.

Amesema katika teknolojia ya akili bandia unacho kiingiza kwenye akili bandia ndicho kitakacho toka na kama ikitumika vizuri itasaidia jamii.

Amesema katika inajiwekeza katika matumizi ya teknolojia kwa kutumia akili bandia na kwamba wao kama wana Azaki wanaunga juhudi hizo kwa kuisaidia Serikali.

"Na sisi tunashauri wananchi waweze kutumia teknolojia katika masuala yanayo leta tija katika masuala ya kimaendeleo na sio jambo lingine ili kwa pamoja tuweze kuijenga nchi kimaadili na kimtazamo"Alisema Fatma

Washiriki wa Mkutano wa Azaki wakiwa kwenye picha ya pamoja .

 Balozi wa Uswis Didier Chasot akizungumza katika Mkutano wa Azaki unaofanyika jijini Arusha.
 

Fatma Fungo afisa mtendaji Mkuu Zanzibar Maisha Bora Foundation akiwa katika Mkutano wa Azaki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...