Na Mwandishi wetu Njombe

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa mkoa wa Njombe pekee, imetoa kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa waendelezaji wa Miradi ya nishati vijijini kama ilivyokuwa kwa Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT - Dayosisi ya Kusini Kati) kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala ambapo Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa ruzuku ya shilingi milioni 997 na mkopo nafuu wa zaidi ya shilingi milioni 922 kupitia Benki ya Maendeleo TIB.

Naibu Waziri wa Nishati ameyasema hayo, Tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala, wilayani Makete, mkoani Njombe.

Naibu Waziri Kapinga amesema, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa kiasi hicho cha fedha kwa waendelezaji wa Miradi ya nishati vijijini ambapo ameitaja Miradi hiyo kuwa ni pamoja na Mradi wa Luponde (Luponde Small Hydro Power Project – unaozalisha KiloWati 900); Mradi wa Uwemba (Uwemba Small Hydro Power Project – unaozalisha KiloWati 840); Mradi wa Matembwe (Ikondo-Matembwe Hydro Power Project – unaozalisha KiloWati 500); na Mradi wa Madope (Madope Small Hydropower Project – unaozalisha MegaWati 1.7).

Aidha; Naibu Waziri Kapinga amesema mkoa wa Njombe unaongoza katika mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa kuwa na miradi mingi ya kuzalisha umeme unatokana na maji na kuongeza kuwa Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekuwa ikinunua umeme huo na kuuingiza kwenye gridi ya taifa kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati ya umeme kwa Watanzania wengi.

Akijibu kuhusu ombi la Askofu Sanga; Mkuu wa Jimbo la Kusini Kati ya KKKT kuhusu ombi la fedha, shilingi milioni 400 ambalo lilitolewa na Askofu huyo kwenda kwa Makamu wa Rais; Mhe. Kapinga amesema jukumu ya REA kuwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya nishati vijijini.

Mhe. Kapinga ameagiza Viongozi wa REA kukutana na Viongozi wa Nishati Lutheran (DKK) Investment Limited ili kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.

“Naelekeza, Watu wetu wa REA, wakutane na Baba Askofu na Wataalam wengine wa Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd ili kuandaa andiko litakalowezesha kupatikana kwa fedha hizo”. Alikaririwa, Naibu Waziri Kapinga.

Naye Mhandisi, Michael Kessy, Meneja wa Teknolojia za Nishati Vijijini kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) amesema kuwa tukio la uzinduzi wa Mradi wa Ijangala umeleta tija kwa taifa kwa kuongeza KiloWati 360 kwenye gridi ya taifa.

Mhandisi Kessy ameongeza kuwa REA imetoa ruzuku ya shilingi milioni 997 na baadae mkopo nafuu wa dola za Marekani 400,000 kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB katika nyakati tofauti kwa ajili ya Mradi wa ueme wa Ijangala.

Mhandisi, Kessy ameongeza kuwa REA ilitoa ruzuku ya milioni 997 kwa awamu tatu; awamu ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya andiko la Mradi pamoja na tathmini ya athari ya mazingira na za kijamii; awamu ya pili ilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme kutoka kwenye kituo cha uzalishaji kwenda kwenye njia ya umeme wa gridi ya taifa ambapo zaidi ya shilingi milioni 426 zilitumika kwa ajili ya ununuzi wa mashine umba (Transformers) mbili, moja kubwa ya KiloVolti 500 na nyengine ndogo; awamu ya tatu zilitolewa dola za Marekani 211,000 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa bwawa na bomba la kusafirisha maji (Penstock) yanayokwenda kwenye kinu cha kufulia umeme.

Mhandisi, Kessy ameongeza kuwa na awamu ya nne ya fedha hizo zilitolewa kupitia mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia ambapo uratibu wa fedha hizo, ulisimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Benki ya Maendelo TIB ambapo jumla ya dola za Marekani 400,000 sawa na shilingi milioni 992 zilitolewa kwa Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala.

 

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akihutubia umati wa watu waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa pamoja na Naibu Waziri Nishati Mhe. Judith Kapinga pamoja na Askofu, Wilson Sanga; Mkuu wa Dayosisi ya Kusini Kati ya KKKT kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala, Makete mkoani Njombe
 

Naibu Waziri Nishati Mhe. Judith Kapinga akiwasalimia Maaskofu wa Dayosisi ya Kusini Kati ya KKKT kwenye eneo bonde la mto ulipo Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala, katika kijiji cha Masisiwe, Makete mkoani Njombe

 

Eneo bonde la mto ulipo Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala, katika kijiji cha Masisiwe, Makete mkoani Njombe wakati Makamu wa Rais alipowasili katika hafla ya  uzinduzi rasmi wa Mradi wa umeme wa maji wa Ijangala, tarehe 27 Oktoba, 2023

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...