Na.Vero Ignatus, Arusha
Serikali ya Tanzania inatekeleza na kisimamia kikamilifu misingi ya haki za binadamu kwa mujinu wa Katiba na kuhakikisha zinatekelezwa na kulindwa kwa mujibu wa mikataba ya Kamisheni za Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mwinyi kwa niaba ya Rais Dkt. Samia wakati akifungua kikao cha 77 cha kawaida cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR)
“Serikali inatekeleza na kusimamia haki za binadamu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo. Katika katiba yetu, haki za binadamu zimeainishwa kuanzia Ibara ya 12 hadi 24 lakini pia Katiba yetu kuanzia Ibara ya 25 hadi 30 imeainisha wajibu wa kila raia.
“Hapa nchini, jitihada mbalimbali zimechukuliwa na Serikali ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kutekelezwa kwa mujibu wa Mikataba ambayo Tanzania ni mwanachama kwa kuwa jitihada hizi zimeboresha hali ya upatikanaji wa haki mbalimbali ikiwemo haki ya usawa mbele ya sheria, afya, elimu, maji na mazingira safi, uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kuabudu, ajira, haki ya kumiliki mali na uhuru wa vyombo vya habari,"alisema.
Amesema kuwa kutokana na uhuru huo, hivi sasa Tanzania ina vyombo vya habari vingi vikiwemo redio 210, televisheni 56, magazeti 288 pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii. Pia, tumefikia hatua kubwa ya kuimarika kwa uhuru wa kidemokrasia, haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Dkt. Mwinyi amesema kuwa suala la ulinzi na uhifadhi wa haki za binadamu katika Bara la Afrika kwa jumla, bado kwa kiasi fulani linakabiliwa na changamoto, Miongoni mwao ni mapinduzi ya Serikali zilizo madarakani, vita vya wenyewe kwa wenyewe, mila na desturi zisizofaa, ukatili wa kijinsia, athari hasi za utandawazi na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu haki zao.
"Natumia fursa hii kutoa wito kwa nchi na Serikali zote wanachama wa Umoja wa Afrika kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto hizi,"alisema"
Tanzania inashiriki katika Jeshi la pamoja la kulinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Pia, kwa muda mrefu imeshiriki katika ulinzi wa amani katika nchi mbali mbali ikiwemo huko Darfur Sudan na Visiwa vya Comoro, yote hayo Ili kuepusha uvunjifu wa haki za binadamu unaotokana na vita, kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Naona fahari kwa Majeshi yetu kwa kazi yao nzuri wanayoifanya. Nitoe wito kwa nchi zetu za Afrika kuendelea kushirikiana katika kuyakabili matukio mbalimbali yanayohitaji msaada wa kibinadamu katika Bara letu," Nawapongeza Makamishina wote wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambao mnashirikiana pamoja katika kuimarisha haki za binadamu na watu katika bara la Afrika"
“Nafahamu kuwa kikao hiki kilitanguliwa na majukwaa ya Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu zipatazo 46 na Asasi za Kiraia takribani 210 kutoka Bara la Afrika. Taasisi hizi ni wadau muhimu katika masuala ya ulinzi, utetezi na uhifadhi wa haki za binadamu barani Afrika. Nakupongezeni sana kwa kuona umuhimu wa kuandaa majukwaa ya Taasisi na Asasi hizo”.
Alisema kwa hakika, changamoto na majanga mbalimbali ambayo bara letu linapitia, wahanga wake wakubwa ni wanawake na watoto hivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua katika kutatua migogoro mbalimbali na kutekeleza kwa vitendo Tamko la Dar es Salaam kuhusu Amani, Usalama, Demokrasia na Maendeleo katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
"Kwa mfano hivi sasa Tanzania inashiriki katika jeshi la Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (Stabilization Mission) na Jeshi la Kulinda Amani (MONUSCO)alisema
“Kwa hakika, kauli mbiu ya siku ya haki za binadamu ya Afrika ya mwaka huu, inanishawishi kuwakumbusha ndugu zangu kutoka Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu, AZAKI na wadau wengine wote mliopo hapa kuwa haki za binadamu tunazozitetea ziwe zinaendana na kauli mbiu hii. Kwa ujumla, Bara la Afrika na Tanzania kwa umahususi wake tunaheshimu haki za binadamu kwa kuzingatia utamaduni, maadili na tunu zetu kama Waafrika,"alisema.
Aidha, ili kuepusha uvunjifu wa haki za binadamu unaotokana na vita, kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inashiriki katika Jeshi la pamoja la kulinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Pia, muda mrefu nchi imeshiriki katika ulinzi wa amani katika nchi mbali mbali ikiwemo huko Darfur Sudan na Visiwa vya Comoro
'Naona fahari kwa Majeshi yetu kwa kazi yao nzuri wanayoifanya Nitoe wito kwa nchi zetu za Afrika kuendelea kushirikiana katika kuyakabili matukio mbalimbali yanayohitaji msaada wa kibinadamu katika Bara letu'.
“Serikali ya Tanzania inaungana nan chi zote za Afrika na wadau wa haki za binadamu katika maadhimisho haya muhimu.Natoa wito kwa Serikali mbalimbali,taasisi za haki za binadamu kuendelea kuchukua hatua za kuimarisha ulinzi na utetezi wa haki za binadamu kwa kushughulikia changamoto zilizoko,”aliongeza Dkt.Mwinyi.
Naye Mwenyekiti wa Kamishna ya ACHPR, Remy Lungu,amesema Tanzania imekuwa kinara wa kudumisha amani ambapo changamoto imekuwa ikitatua yenyewe bila ya kuwapo kikwazo hivyo amezitaka nchi nyingine kuiga mfano huo.
“Hakuna maendeleo bila haki na hatuwezi kuwa na Amani bila maendeleo hivyo haki ni wajibu kwa wanachama,”alisema.
Kwa upande wake Msajili wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,Dkt.Robart Eno,akizungumza kwa niaba ya Rais wa Mahakama hiyo, Jiji Iman Abood, alisema tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo miaka 16 iliyopita imeshatoa maamuzi 100,lakini ni mashauri sita pekee nchi hizo zimefanikiwa kutekeleza.
Aidha kikao hicho cha kawaida kimebebakauli mbiu isemayo chenye kauli mbinu ‘'Kuimarisha na Kuendeleza Utamaduni wa Haki za Binadamu kwa Nyakati zijazo’'
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...