Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefanya ziara katika Chuo Kikuu cha Utalii na Urithi wa Utamaduni ( International University of Tourism and Cultural Heritage) na kujionea mafunzo yanayotolewa na sambamba na nyenzo za kufundishia.
Akizungumza na Mkuu wa Idara ya Utalii katika chuo hicho leo Oktoba 20, 2023, Mhe. Kairuki ameeleza nia ya kuanzisha ushirikiano kati ya Chuo hicho na Vyuo vya Tanzania vinavyotoa mafunzo ya utalii na ukarimu.
Naye, Mkuu wa Idara ya Utalii wa Chuo hicho, Bw. Akmal Odilov alieleza kuwa ni Chuo cha kimataifa na chenye Wahadhiri wabobezi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Aidha, aliongeza kuwa wako tayari kushirikiana na Tanzania katika kuboresha mitaala, kubadilisha wahadhiri sambamba na wanafunzi kutoka pande zote mbili.
Vilevile, alieleza kuwa Chuo hicho hutoa ufadhili wa Shahada ya Pili katika fani za Utalii na Ukarimu na watatoa kipaumbele kwa Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...