Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) inatekeleza Mradi wa ufungwaji wa mitambo ya Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Sauti kati ya Rubani na Mwongoza ndege yaani VHF Radio Communication Systems ili kuboresha huduma ya Uongozaji Ndege katika Anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii ikiwa na lengo la kuboresha mawasiliano katika anga la Tanzania.


Akizungumza wakati wa kupokea mitambo hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari amesema mradi huu unatakelezwa kwa ufadhili wa Serikali kuu kwa fedha za kitanzania bilioni 31.5 ambapo Mamlaka iliandaa mahitaji yaani specification na kutangaza tenda shindanishi ambapo Kampuni ya Jotron AS ya Nchini Norway ilishinda zabuni na kuingia nayo mkataba June 2022 na kuanza utakelezaji wake mara moja.

"Leo ninayofuraha kuwataalifu kuwa mitambo yote imefika hapa katika bandari ya Dar es salaam ikiwa na shehena ya makontena 10 yenye urefu wa futi arobaini(40 feet) ikitokea Milano nchini Italy na Oslo nchini Norway" Alisema Johari 

Pia amasema Mitambo hii itasafirishwa na kusambazwa katika meaneo yote yanayopitiwa na mradi huo ambapo itasimikwa katika viwanja vya ndege kumi na mbili (12) ambavyo ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), Uwanja wa Ndege wa Pemba, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA), Uwanja wa Ndege wa Songwe ,Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Tabora, Uwanja wa Ndege wa Kigoma, Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Uwanja wa Ndege wa Tanga, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) na Uwanja wa Ndege wa Arusha.

Amesema pamoja na maeneo hayo mitambo itafungwa katika maeneo ya kurefusha na kukuza Mawasiliano ya sauti kwa anga la juu (yaani VHF extended Relay stations) katika vituo kumi na nane(18) nchi nzima ambayo ni Kaluwe (Mbeya), Matogoro (Songea), Nambunga (Mtwara), Mwaseni (Rufiji –Pwani), Michakaini (Chakechake-Pemba), Lolkisale (Arusha) Oldean Malanja (Ngorongoro –Arusha), Kwenjugo (Tanga), Gairo (Morogoro), Ngoli (Dodoma), Lubuli (Dodoma), Mwisi (Tabora), Moroninya (Kasulu-Kigoma), Nyamanyama (Biharamulo-Kagera), Ndisso-Sitalike (Katavi), Kitulo (Njombe), Muganza (Butiama-Mara) na Mugumu Town (Serengeti-Mara)

Amesisitiza kuwa Mitambo hii pia itafugwa kwenye kituo cha mpango wa dharura wa uongozaji ndege kwa masafa mafupi na ya kati (yaani Dar backup centre for aerodrome and Approach control) katika kiwanja cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na ufungwaji wa mitambo kwenye kituo cha dharula kwa mawasiliano ya anga la juu (yaani Area control centre) katika kiwanja cha ndege cha Mwanza.

Mitambo iliyopokelewa leo katika bandari ya  Dar es Salaam ni Redio za Kidigitali za Masafa ya juu (yaani VHF Digital Radios), Mitambo ya kurekodi mifumo ya Mawasiliano ya sauti (Digital Voice Recording Systems) na Mifumo ya kuunganisha na kuangalia mifumo ya mawasiliano (Voice Switching Systems VCCS) ambapo Ufungwaji wa mitambo hii utachukua miezi minne ambapo tunatarajia kuwasha rasmi mwezi April 2024 na kuaza kutoa huduma katika Anga lote ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwasili kwa mitambo ya Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Sauti kati ya Rubani na Mwongoza ndege yaani VHF Radio Communication Systems iliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuboresha huduma ya Uongozaji Ndege katika Anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wa kwanza kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA,Bw. Daniel Malanga na kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce.
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na waandishi wa habari wakati wa kupokelewa kwa mitambo ya Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Sauti kati ya Rubani na Mwongoza ndege yaani VHF Radio Communication Systems iliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuboresha huduma ya Uongozaji Ndege katika Anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari akiangalia baadhi ya mitambo ya Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Sauti kati ya Rubani na Mwongoza ndege yaani VHF Radio Communication Systems iliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuboresha huduma ya Uongozaji Ndege katika Anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya  mitambo ya Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya Sauti kati ya Rubani na Mwongoza ndege yaani VHF Radio Communication Systems viliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuboresha huduma ya Uongozaji Ndege katika Anga la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...