Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak amesema madhumuni ya kikao hicho ni kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa COP28 huku masuala ya Uchumi wa Buluu yatakuwa ni ajenda muhimu.
Nae, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius ametaja lengo kuu la wajumbe hao kukutana jijini Arusha ni kujadili kwa pamoja yaliyojiri kwenye COP27 iliyofanyika nchini Misri mwaka 2022 mafanikio, changamoto na mwelekeo kuelekea COP28.
Aidha Mkutano huo wa ( COP28) utakaofanyika Dubai,Umoja wa Falme za Kiarabu kuanzia Novemba 30 hadi Decemba 12,2023 Ambapo msimamo wa nchi ni kuwa na lugha moja katika suala hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...