Na Karama Kenyunko Michuzi TV
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imetangaza kufungua awamu ya nne na ya mwisho ya udahili ngazi ya shahada ya kwanza katika taasisi ya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kuanzia leo Oktoba 13, 2023 hadi Oktoba 17mwaka huu.
hatua hiyo inatokana na tume hiyo kupokea maombi ya kuongezwa muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu za tatu zilizopita na vyuo ambavyo vina nafasi.
Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa udahili wa awamu tatu na kuonekana kuna baadhi ya wanafunzi hawakuweza kukamilisha udahili wao katika dirisha la kwanza hadi la tatu huku baadhi ya vyuo ambavyo bado vina nafasi vikiomba kupewa muda wa kuendelea kudahili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 13, 2023 Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema lengo la kufunguliwa kwa dirisha la nne ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha, Profesa Kihampa amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahili ama kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU kuanzia leo Oktoba 13 hadi Oktoba 24, 2023 kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Profesa Kihampa amesema mpaka kukamilika kwa dirisha la tatu waombaji waliopata udahili ni 130,000 kati ya waombaji 142,440 huku vyuo vikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 187,084

Katibu Mtendaji wa tume ya vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la nne na la mwisho la udahili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa mwaka wa masomo 2023/2024 Jijini Dar es Salaam.


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...