TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Kituo cha Urithi wa Ukombozi Bara la Afrika wanashiriki Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni linalofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa) mjini Bagamoyo lililoanza kuanzia Oktoba 26 mwaka 2023 .
Katika tamasha hilo wadau mbalimbali wameombwa kutembelea katika banda la TET kwa lengo la kuangalia machapisho mbalimbali yanayotolewa na taasisi hiyo.
Akizungumza katika maonesho hayo,Ofisa Uhusiano wa TET Angella Msangi ameleeza katika tamasha hilo , wadau watapata kuona vitabu vya historia vilivyoandaliwa na TET vilivyoshirikisha wataalamu bobezi katika kufundisha somo la historia kutoka Taasisi mbalimbali.
“Mje mjione mauudhui yaliyomo kwenye vitabu hivyo ambayo yamelenga kumwezesha mwanafunzi kupata umahiri wa kuijua historia ya nchi yake na ya mahusiano ya Tanzania na nchi nyingine”. Amesema Anngella.
Pia, mwanafunzi atapata nafasi ya kujua historia iliyo nje ya Tanzania na hasa bara la Afrika na kufahamu masuala mbalimbali.
Pamoja na hayo, katika tamasha hilo wananchi wataweza kuona machapisho mbalimbali yanayotolewa na kufahamu kazi zinzofanywa na TET kwa ujumla.
Tamasha hilo linatarajia kumalizika Oktoba 28, 2023 ambapo washiriki mbalimbali kutoka katika taasisi za binafsi za Serikali na nje ya nchi zinaashiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...