NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WAZIRI wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Tamsha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Bagamoyo Festival) ambalo litafanyika Oktoba 26,2023 kwenye Viwanja vya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 25,2023, Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamomoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye amesema katika tamasha hilo, vikundi 45 vya sanaa ambapo 34 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar huku vingine vikitoka nchi mbalimbali vitashiriki kuonesha umahili wao katika sanaa.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuvutia wadau wa sanaa kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo kutangaza utamaduni na vivutio mbalimbali ambavyo vinapatikana kwenye maeneo tofauti tofauti.

"Tamasha la mwaka huu kutakuwa maonyesho ya wajasiriamali ambayo yatahusisha taasisi 15 za serikali na sanaa za ufundi zitashirikisha washiriki 30 na pia washiriki watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Wilaya ya Bagamoyo vikiwemo Mji Mkongwe, Kaole na Boma la Wajerumani". Amesema Dkt. Makoye.

Pamoja na hayo Dkt. Makoye amesema kuwa nchi zilizothibitisha kushiriki tamasha la hilo msimu huu wa 42, ni pamoja na nchi ya Canada, Botswana, Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Burundi na Kenya.


Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamomoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 25,2023 Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu kuelekea uzinduzi wa Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 26,2023 na mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...