Na John Mapepele


Wizara ya Maliasili na Utalii kwa  kushirikiana na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo leo zimekutana  kutekeleza  maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan ya kuandaa mkakati wa pamoja wa kufungamanisha  utalii na utamaduni ili kuongeza pato la taifa.


Katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara  hizo, Dkt. Hassan Abbasi (Maliasili na Utalii) na Gerson Msigwa (Utamaduni, Sanaa na Michezo)  na kuhudhuriwa na  watendaji wa sekta hizo  wameazimia kuainisha maeneo  muhimu ya kushirikiana  ili yatumike kutangaza  utalii ambapo pia imeundwa timu ya kuandaa mkakati huo na  bajeti yake.

Akifungua kikao hicho Dkt. Abbasi amefafanua kwamba kutokana na kushabihiana kwa malengo ya Wizara hizi mbili Viongozi Wakuu wa Taifa wakiwemo Mhe. Rais, Mhe. Makamu wa Rais na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameelekeza kuwepo kwa ushirikiano katika uendeshaji wa shughuli za sekta kwa manufaa  ya taifa.


Dkt. Abbasi amesema kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia katika Tamasha la Utamaduni Viwanja vya Red Cross Mwanza Septemba 8, 2021, alisisitiza, utamaduni ni biashara na chanzo kikubwa cha mapato, hivyo ni muhimu kutekeleza kwa nguvu kubwa katika kukuza utalii wa kitamaduni.


“Utalii wetu umejikita zaidi kwenye maliasili, wanyamapori, misitu, fukwe milima na mambo mengine, na hii pia inachangia watalii wanaokuja nchini kukaa siku chache; idadi ya siku ambazo watalii hukaa nchini ni ndogo mno, lakini tungekuwa na matamasha ya aina hii wangezunguka na kuona na kujifunza. Na hii ndio maana, Serikali imejipanga kuongeza wigo wa vivutio vya utalii, ukiwemo utalii wa kiutamaduni”. Alisema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zina wadau na matukio maarufu wenye mvuto na ushawishi mkubwa katika jamii ndani na nje ya nchi na hivyo kutoa fursa kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Aidha, amefafanua kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya asili na vya kitamaduni kama vile fukwe za Bahari ya Hindi, maziwa, mito, milima, mabonde, wanyamapori, misitu mikubwa ya asili, tamaduni za kipekee kutoka kwa jamii zaidi ya 120

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...