Na WAF - Luanda, Angola.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu  amemuwakilisha  Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu  katika mkutano wa Jumuiya ya SADC wa Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya UKIMWI unaoendelea  Luanda Nchini Angola kuanzia Novemba 25 - 29,2023.            

Awali Dkt. Jingu ameshiriki Uzinduzi  wa Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya matembezi na maandamano kwa washiriki kubeba mabango yenye jumbe mbalimbali zenye Kaulimbiu isemayo "Community led" uzinduzi ambao ni sehemu ya nchi za Jumuiya ya SADC kushirikiana na nchi mwenyeji kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI miongoni mwa nchi wanachama.

Katika Mkutano huo, Mawaziri na wawakilishi wao wanatarajiwa kujadili masuala ya afya yenye lengo la kuchangia katika kufanikisha uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi katika nchi wanachama, kuchunguza hali ya utekelezaji wa maamuzi ya vikao vyao vya pamoja vya awali na kupitia hali ya afya katika ukanda wa SADC.

Mawaziri wa afya pia watahudhuria maadhimisho ya Siku ya Malaria ya SADC Luanda - Angola tarehe 29 Novemba 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...