Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.
Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya
kufanya mahojiano maalumu kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya
Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid-Term Review)
utakaofanyika Zanzibar, kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023,
ukiwashirikisha wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa takribani 100
duniani.
Katika mahojiano hayo, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi, amewakaribisha washiriki wa mkutano huo nchini Tanzania hususan, katika Visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar), ili kushuhudia Maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii yaliyofikiwa kupitia mikopo nafuu na misaada kupitia Benki ya Dunia na amewataka wananchi kuchangamkia fursa za ugeni huo katika Sekta mbalimbali ikiwemo utalii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...