Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Shirika la Maendeleo ya Tafsiri ya Lugha ya Alama Tanzania (TSLTDO) wamesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kikazi wenye lengo la kusaidia wanafunzi Viziwi kupata elimu kwa kuwa na vifaa bora vya kujifunzia na kufundishia kama walivyo wanafunzi wengine.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameeleza kuwa makubaliano hayo ya ushirikiano ambapo baadhi ya maeneo hayo ni TET itawakutanisha TSLTDO na Wakuza Mitaala kwa ufafanuzi wa jambo lolote iwapo itahitajika kufanyika hivyo.
Maeneo mengine ni TET kutoa usaidizi wa kitaalamu katika kutathmini usahihi wa ufasiri wa vitabu uliofanywa na TSLTDO kadiri itakavyohitajika pamoja na kutoa fedha zitakazowezesha kukamilisha zoezi la kutafsiri vitabu vya kiada kwa mujibu wa taratibu na kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.
“TET, kwa upande wetu tunayo mategemeo makubwa kuwa ushirikiano huu utatupelekea kutekeleza majukumu yetu na utatusaidia kuongeza wigo kwa kuwafikia kundi lingine la wanafunzi wenye mahitaji maalumu na hivyo kuwawezesha wanafunzi viziwi kupata vifaa bora vya ujifunzaji na ufundishaji bila kikwazo chochote”, amesema Dkt. Komba.
Kwa upande wake, Rais wa TSLTDO, Mch.Sensor Msimbete ameeleza kuwa ni jambo kubwa mno kwa wanafunzi viziwi sasa kuwa na vitabu ambavyo watakuwa na uelewa navyo. Pia, ameishukuru Serikali kwa ujumla kupitia TET kwa kukubali kutafsiri vitabu vyote vya kiada kwa wanafunzi viziwi hapa nchini.
“Hili ni jambo muhimu na kubwa kwetu jamii ya viziwi nchini, kwani sasa kwa wanafunzi wetu ni ukombozi mkubwa kwa wao kuweza kuelewa zaidi masomo darasani kutokana na kupatikana kwa vitabu vitakavyoandakwa kwa lugha wanayoielewa” amesema Mch.Msimbete.
Naye ,Mkurugenzi wa Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Magreth Matonya amesema kuwa, ni jambo la muhimu na la kihistoria kwa nchi kwani hii ni fursa pekee kwa wanafunzi viziwi sasa kuweza kusoma na kuelewa zaidi kwa kuwa na vitabu vitakavyokuwa na lugha wanayoilewa.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt.Aneth Komba na Rais wa Shirika la maendeleo ya Tafsiri ya lugha ya Alama Tanzania(TSLTDO) Mchungaji Sensor Msimbete wakionesha hati za makubaliano ya ushirikiano wa kikazi wenye lengo la kusaidia wanafunzi viziwi nchini ili kupata elimu kwa kuwa na vifaa bora vya kujifunzia na kufundishia kama walivyo wanafunzi wengine.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt.Aneth Komba na Rais wa Shirika la maendeleo ya Tafsiri ya lugha ya Alama Tanzania(TSLTDO) Mchungaji Sensor Msimbete leo Novemba 3,2023 jijini Dar es Salaam wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano wa kikazi wenye lengo la kusaidia wanafunzi viziwi nchini ili kupata elimu kwa kuwa na vifaa bora vya kujifunzia na kufundishia kama walivyo wanafunzi wengine.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt.Aneth Komba na Rais wa Shirika la maendeleo ya Tafsiri ya lugha ya Alama Tanzania(TSLTDO) Mchungaji Sensor Msimbete wakibadilishana Hati za makubaliano ya ushirikiano wa kikazi wenye lengo la kusaidia wanafunzi viziwi nchini ili kupata elimu kwa kuwa na vifaa bora vya kujifunzia na kufundishia kama walivyo wanafunzi wengine.
.jpeg)

.jpeg)
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameeleza kuwa makubaliano hayo ya ushirikiano ambapo baadhi ya maeneo hayo ni TET itawakutanisha TSLTDO na Wakuza Mitaala kwa ufafanuzi wa jambo lolote iwapo itahitajika kufanyika hivyo.
Maeneo mengine ni TET kutoa usaidizi wa kitaalamu katika kutathmini usahihi wa ufasiri wa vitabu uliofanywa na TSLTDO kadiri itakavyohitajika pamoja na kutoa fedha zitakazowezesha kukamilisha zoezi la kutafsiri vitabu vya kiada kwa mujibu wa taratibu na kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.
“TET, kwa upande wetu tunayo mategemeo makubwa kuwa ushirikiano huu utatupelekea kutekeleza majukumu yetu na utatusaidia kuongeza wigo kwa kuwafikia kundi lingine la wanafunzi wenye mahitaji maalumu na hivyo kuwawezesha wanafunzi viziwi kupata vifaa bora vya ujifunzaji na ufundishaji bila kikwazo chochote”, amesema Dkt. Komba.
Kwa upande wake, Rais wa TSLTDO, Mch.Sensor Msimbete ameeleza kuwa ni jambo kubwa mno kwa wanafunzi viziwi sasa kuwa na vitabu ambavyo watakuwa na uelewa navyo. Pia, ameishukuru Serikali kwa ujumla kupitia TET kwa kukubali kutafsiri vitabu vyote vya kiada kwa wanafunzi viziwi hapa nchini.
“Hili ni jambo muhimu na kubwa kwetu jamii ya viziwi nchini, kwani sasa kwa wanafunzi wetu ni ukombozi mkubwa kwa wao kuweza kuelewa zaidi masomo darasani kutokana na kupatikana kwa vitabu vitakavyoandakwa kwa lugha wanayoielewa” amesema Mch.Msimbete.
Naye ,Mkurugenzi wa Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Magreth Matonya amesema kuwa, ni jambo la muhimu na la kihistoria kwa nchi kwani hii ni fursa pekee kwa wanafunzi viziwi sasa kuweza kusoma na kuelewa zaidi kwa kuwa na vitabu vitakavyokuwa na lugha wanayoilewa.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt.Aneth Komba na Rais wa Shirika la maendeleo ya Tafsiri ya lugha ya Alama Tanzania(TSLTDO) Mchungaji Sensor Msimbete wakionesha hati za makubaliano ya ushirikiano wa kikazi wenye lengo la kusaidia wanafunzi viziwi nchini ili kupata elimu kwa kuwa na vifaa bora vya kujifunzia na kufundishia kama walivyo wanafunzi wengine.
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...