Kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia imeanza leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila.
Kambi hiyo inaendeshwa na Prof. Mamoun Gadir kutoka Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza, kwa kushirikiana na wataalamu wa Mloganzila.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji MNH-Mloganzila Dkt. Godlove Mfuko amesema katika siku ya kwanza jumla ya wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji na katika siku tano za kambi watu 35 watanufaika na upasuaji huo.
Aidha, amebainisha kuwa kambi itaendelea hadi Disemba Mosi mwaka huu na baada ya kambi utaratibu wa kawaida wa matibabu hayo utaendelea ambapo wagonjwa wataendelea kuhudumiwa na wataalamu wazalendo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...