Na Mwandishi wetu Kongwa - Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii inaendeleza jitihada za kuhifadhi vyema maeneo yenye historia adhimu nchini yakiwemo majengo na mahandaki yaliyotumiwa na wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Afrika Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma, ili yaweze kuongeza tija katika sekta ya Utalii.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, kwenye Mbio za hiyari zijulikanazo kama Kongwa: African Liberation Marathon, Mhifadhi Mkuu Idara ya Malikale Bi. Prisca Kirway amesema Wilaya ya Kongwa ina utajiri mkubwa wa Malikale ambao ni kielelezo muhimu cha Kitaifa na Kimataifa ya namna Tanzania ilivyoshiriki kikamilifu katika Harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, maeneo ya kihistoria Wilayani humo ni lazima yalindwe kwa mujibu wa sheria.

“Kama Wizara, eneo hili la Kongwa ni muhimu sana kwa kutunza urithi wa Kihistoria na Utalii, Hivyo kwa umuhimu huo Wizara imefanya jitihada za kuhakikisha eneo hili linaingia katika Orodha ya Maeneo ya Urithi wa Taifa kwa kupewa Tangazo la Serikali- GN ili lilindwe na kuhifadhiwa kisheria”. Alisema Bi Kirway

Bi Kirway ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kongwa kwa kutumia Utalii wa Michezo kupitia Kongwa: African Liberation Marathon) na Historia adhimu ya Harakati za Kupigania uhuru Barani Afrika kama fursa ya kujitangaza kiutalii na kuahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini katika uhifadhi wa maeneo yaliyobeba urithi wa Kihistoria.

Akizungumzia Mbio hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema, amesema, lengo la mbio hizo ni kuijulisha Dunia na kurithisha kizazi kilichopo, kupitia Michezo Historia ya mchango mkubwa wa Tanzania katika ukombozi wa Bara la Afrika kupitia Wilaya ya Kongwa.

Mbio hizo za hiyari, zimezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe Jerald Mongela kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa naMichezo Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro, na kusisitiza kuwa zitakuwa zikikimbiwa kila Mwaka.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...