Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Nchini (TGDC), imeanza safari za uzalishaji wa umeme wa kutumia jotoardhi katika eneo la Ngozi lililoko Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambapo zaidi ya megawati 70 zitazalishwa kutoka eneo hilo.

Katika ziara iliyofanyika Novemba 23, 2023, ikiihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Rungwe ambayo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Jaffar Haniu alisema kuwa ziara hiyo ni muhimu kwa kamati hiyo kupata uelewa juu ya mradi huo.

“Ziara hii imeweza kutupa manufaa na uelewa juu ya mradi mzima ambao unatekelezwa hapa na hii itatufanya sisi kuwa mabalozi wazuri wa mradi huu na tutaweza kuusemea mradi huu na kuhakikisha kuwa tunaulinda”, alisema Jaffar Haniu.

Haniu alisema kuwa Mradi huo ni wa kitaifa na anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuupa nguvu mradi huo kwa kutoa fedha na watalaam kwani utekelezaji wa mradi huo utapunguza adha ya umeme nchini.

Aidha, Haniu alisema utekelezaji wa mradi huo wa uzalishaji umeme katika eneo la Ngozi utakuwa moja ya suluhisho la upatikanaji wa umeme nchini kama ilivyo kwa nchi nyingine wanaotumia chanzo hicho cha nishati kuzalisha umeme.

Kwa upande wake Maneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Mathew Mwangomba alisema kuwa Tanzania ina maeneo mengi ya nishati ya jotoardhi lakini katika kuweka kipaumbele maeneo Matano yako kwenye mpango wa kwanza wa uzalishaji umeme kupitia nishati ya jotoardhi.

“Katika miradi yetu ya kipaumbele eneo hili la Ngozi ni majowapo ya maeneo muhimu ya kuzalisha umeme wa jotoardhi, Tanzania tuna rasilimali ya jotoardhi megawati 5000 na megawati 15000 za joto ambazo zinaweza kuzalishaji umeme na kutumika katika sekta nyingine za uzalishaji ikiwemo kilimo na ufugaji”, Alisema Mwangomba.

Aliongeza kuwa katika eneo la Ngozi ambalo lipo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya linauwezo wa kuzalisha megawati 70 ambapo katika hatua ya Awali Serikali kupitia TGDC itaanza na uzalishaji wa mgewati 30 za umeme, pia kwa sasa eneo hilo limefungwa mtambo wa kuchoronga kisima ambao utachoronga kwa takribani siku 45 hadi 65 ili kuwezewesha utafiti zaidi.

Naye, Maneja Mradi wa Ngozi, Fatumati Mnzava ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Mbeya hasa Wilaya ya Rungwe ambapo mradi huo unatekelezwa kwani wamekuwa wakishirikiana nao kuanzia hatua za mwanzo za utafiti mpaka sasa ambapo mitambo ya uchorongaji visima imefungwa.

“Kipekee nitoe shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Mbeya hasa kwa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe kwa kutupa ushirikiano mkubwa tangu tuanze mradi huu kwani tunategemea kuchimba visima vitatu kati kabisa is a kata za Wilaya hii ambapo cha kwanza ni kata ya Isongole, Swaya na Iongwe juu”, Alisema Fatumati Mnzava.

Diawani wa Kata ya Isongole, Bwana Mwalingo Sothe, ambako mtambo umefungwa tayari kwa kuanza kazi ya uchorongaji ameishukuru Serikali kupeleka mradi huo katika kata yake kwani wamenufaika na upatikanaji wa maji katika shule ya msingi Mbeye 1 ambapo wanafunzi walikuwa wanalazimika kuchota maji mto kiwira ambayo hayakuwa salama.

“Serikali ina nia nzuri ya kutuletea mradi huu tulikuwa na changamoto ya maji katika shule ya msingi Mbeye 1 wanafunzi walikuwa wanakatiza barabara kwenda kuchota maji mto kiwira na walikuwa wakipata ajali mara kwa mara na yale maji hayakuwa salama kwao lakini TGDC wameweka tanki la maji shuleni hapo na kuepusha Watoto wetu kupata adha ya maji” alisema Mwalingo Sothe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...