Mashindano ya Safari Lager Cup yanayodhaminiwa na Bia ya Safari Lager, yamezidi kunoga huku timu nne zikitangazwa.

Msemaji wa mashindano hayo, yaliyoleta msisimko wa aina yake, Mbwiga Mbwiguke, alisema zoezi hilo la kuibua vipaji, liliendeshwa k iwa ukamilifu kama ilivyopangwa na tayari wachezaji 22 kutoka kila Mkoa wameshachaguliwa.

"Kama tulivyowaarifu hapo awali, zoezi hili lilishirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha na hatimaye Dar es Salaam ambapo makocha mahiri Jamhuri Kihwelo na Sekojo Chambua walikuwa na kazi ngumu ya kuchagua kikosi Cha wachezaji 22 kutokana na bonanza mbalimbali walizoshiriki baada ya usaili,"alisema.

Alisema hatua inayofuata sasa ni timu hizo nne kushindanishwa na Kisha makocha watachagua timuu moja itakayojulikana kama Safari Lager Champions ambayo hatimaye itacheza na timu mojawapo ya Ligi Kuu Tanzania.

Meneja wa Bia ya Safari Lager Pamela Kikuli, aliwapongeza makocha Jamhuri Kihwelo na Sekojo Chambua Kwa kuendesha zoezi Hilo Kwa weledi mkubwa na kutumia uzoefu wao kuchagua timu hizo.

Alisema bia ya Safari, ambayo ni ya mabingwa iliamua kuja ya kampeni hii ili kuibua vipaji vipya kabisa vya mpira wa miguu kwani wanaamini kuna vipaji vingi nchini ambavyo havijaibuliwa.

Aliongeza kuwa hatua inayofuata itakuwa na msisimko mkubwa kwani timu nne zilizochaguliwa zitachuana ili kupata timu moja ya wachezaji 22 itakayocheza na timu ya Ligi Kuu.

Kocha Kihwelo alisema zoezi limefanikiwa Kwa asilimia 90 hasa ikizingatiwa kuwa ndio mara ya kwanza na waliojitokeza walikuwa wengi zaidi na wao kama makocha walikuwa na kibarua kigumu kuchuja kwani katika mikoa yote minne kulikuwa na vipaji vya kipekee.

"Sio kwamba walioachwa ni wabaya, ni kwba tu walihitajika 22 lakini kiwango Cha vipaji Kiko juu na tunaishukuru Safari Lager Kwa kuona umuhimu wa kuibua vipaji vya mpira wa miguu kwani wengi walikuwa wanakosa nafasi ya kutoka," alisema na kutoa wito Kwa vilabi mbalimbali vyenye programu ya U-20 kuwatumia vijana walioachwa Kwa kuwa wana vipaji vya hali ya juu.

Kocha Chambua alisema zoezi Hilo lilikuwa ya aina yake kwani limedhihirisha kuwa kuna vipaji vya hali ya juu katika mikoa mbalimbali na kutoa wito Kwa makampuni mengine yaige mfano wa Safari Lager na kutenga fedha na rasilimali Kwa ajili ya kuibua na kukuza vipaji.

"Zoezi lilikuwa gumu maana Kuna vipaji vya hali ya juu. Tulitamani tuwachukue wote lakini nafasi zilikuwa 22 tu Kwa kila Mkoa. Tumearifiwa kuwa zoezi hili ni endelevu Kwa hivyo tunaamino mwakani litakuwa kubwa zaidi ili Safari Lager iendelee kuibua vipaji zaidi.

Bia ya Safari Lager imewahi kudhamini mashindano ya Taifa Cup ambayo yalishirikisha mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kuibua vipaji. 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...