Na Mwandishi Wetu

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewapongeza wahitimu bora wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) cha Morogoro kwa kuwapatia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni Tano (5)

Motisha hiyo ya fedha, imetolewa na TADB kama sehemu ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kupitia mpango mkakati wake mpya uliozinduliwa mwaka huu.

Akiongea wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri na wafanyakazi katika eneo la utafiti, Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa TADB Bi. Jacqueline Minja alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Benki yetu inatambua uwepo wa mikakati mbalimbali ya serikali kama vile sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 ambayo imetilia mkazo umuhimu wa kuweka mazingiza wezeshi kwa vijana kujihusisha na shughuli za kiuchumi, ikiwemo kilimo cha kisasa na kibiashara. Kwa kutambua hili, kwa kuanza, TADB imefika hapa na kutoa tuzo kwa wanafunzi bora mwaka huu.”

Afisa rasilimali huyo alieleza kuwa, katika awamu nyingine, benki itaandaa programu maalumu ya kuatamia vijana bora kutoka chuo kikuu cha SUA ilikutoa fursa ya kujifunza kazini.

“Programu hiyo itakayokuwa ya miezi 24, italenga kutoa nafasi kwa wahitimu bora kuweza kupata nafasi ya kujifunza kazi kwa vitendo katika benki yetu,” Alieleza Bi. Minja.

Akizungumza katika mahafali hayo, Kaimu Mkuu wa Chuo Prof Raphael Chibunda aliishukuru TADB kwa kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri pamoja na mpango wake wa kuandaa programu maalum ya kuwaatamia wahitimu wa fani ya kilimo.

TADB itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) katika juhudi za kutengeneza vijana wabobezi katika sekta ya kilimo ili kuwezesha vijana kuchangia kufikia malengo ya serikali ya ‘Agenda 10/30’.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kampasi kuu Morogoro, Prof Raphael Chibunda (katikati) akiongea na Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa  TADB na SUA ofisini kwake.

Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro Prof Raphael Chibunda muda mfupi baada ya kumtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya namna taasisi hizo mbili zinaweza kuendelea kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ( wa pili kushoto) , Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (wa tatu kushoto), wakikabidhi mfano wa hundi kwa wahitimu bora Kumi (10) wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA). Wanaoshuhudia kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo SUA Prof Raphael Chibunda na kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa TADB.

 

Wafanyakazi wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu bora wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 5 kwa wanafunzi hao kuwapongeza kwa juhudi walizoonesha katika masomo yao.

Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (katikati) akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 5 kwa wanafunzi hao ikiwa ni kama motisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...