Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameelekeza kuondolewa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Bw. Stephen Lukanga baada ya kushindwa kupanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini.

Waziri Ulega ametoa maamuzi hayo wakati akikabidhi maboti (11) yenye thamani ya Shilingi ya Bilioni 1. 85 yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 28, 2023.

Waziri Ulega amefika maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa Uvuvi Mkoani Dar es Salaam ya kukithiri kwa vitendo vya Uvuvi haramu katika ukanda Pwani hususani Dar es Salaam.

Oktoba 4, 2023 akiwa mkoani Mwanza katika Soko la Lumumba, Waziri Ulega alimtaka Kaimu Mkurugenzi huyo kuwa ndani ya Mwezi mmoja kuhakikisha anapanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini ambao kwa muda umekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi.

Kufuatia kushindwa kutekeleza mikakati hiyo, Waziri Ulega ameamua kumuondoa katika nafasi hiyo na kuelekeza nafasi hiyo apewe aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohamed Sheikh.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...