Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Kifedha Y9 Microfinance Fredrick Mtui (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya saba kwa njia ya simu Anorld Jacob na Jekapo ambaye amejishindia simu janja wote ni wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa Y9 kutoa zawadi kila wiki Kwa wateja wake. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani ni Meneja Masoko ya Taasisi hiyo Bi. Sophia Mang'enya pamoja na mshindi wa pikipiki Wa droo ya sita Bw Baraka Bazarae (kushoto).

Meneja Masoko ya taasisi Bi Sophia Mang'enya akimkabidhi zawadi ya pikipiki mmoja kati ya washindi wa droo ya sita Baraka Bazarae katika hafla ya uchezeshwaji wa droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa pikipiki Droo ya sita ya Y9 Microfinance Baraka Bazarae Katikati akizungumza wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Fredrick Mtui (kulia) na Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi (kushoto).

Meneja Masoko ya Taasisi ya Kifedha ya Y9 Microfinance Bi Sophia Mang'enya (kulia), akimkabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita Baraka Bazarae ambae aliibuka kidedea wakati wakuchezesha droo ya sita wiki iliyopita  makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa yakuchezesha droo kwaajili  ya kutafuta washindi wa droo ya Saba. Kushoto ni Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi (kushoto).


Washindi wa Droo ya saba ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Anorld Jacob na mshindi wa simu Jekapo wote wakiwa ni wakazi wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji taasisi ya kifedha Y9 microfinance Fredrick Mtui ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.

Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ilikuwa ni kuhakikisha  kuwa kila mteja wa Y9 microfinance anapata nafasi ya kushiriki na kushinda katika droo inayochezeshwa kila wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...