Na Mwandishi Wetu
MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimhali ya Jiji la Dar es Salaam zimeanza kuleta madhara kwa wakazi wa maeneo hayo yakiwemo ya kuharibu miundombinu huku daraja la Kigogo na Jangwani mawasiliano ya barabara yamekatika.
Kutokana na mvua hizo Michuzi TV na Michuzi Blog imeshuhudia maeneo mbalimbali ya Jiji hilo baadhi ya nyumba zikiwa zimezingirwa na maji kiasi cha kubaki paa.
Baadhi ya nyumba zilizopo pembezoni mwa bonde la Mto Msimbazi zinaonekana kuwa hatarini kwani maji yamejaa na kuathiri kuta za nyumba.
Maeneo kama Kigogo wananchi wameonekana wakiteka maji ndani ya kuyatoa nje baada ya mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia leo kusababisha maji kujaa ndani.
Aidha maeneo kama ya Kawe jijini Dar es Salaam nako mvua zimesababisha maeneo mengi kuzingirwa maji na kuzua hofu kwa wananchi hasa wanaonekana kuwa kwenye mikondo inayopitisha maji.
Tegeta kwa Ndevu nako mvua zimesababisha athari kwa baadhi ya wakazi baada ya nyumba zao kuathiriwa na maji kiasi cha kuondoa udongo unaoshikilia kuta za nyumba , hivyo iwapo mvua zitaongezeka zinaweza kusababisha madhara zaidi.
Katika maeneo mengine ya jijini Dar es Salaam mawasiliano ya barabara yameanza kuharibika kutokana na maji kujaa na hivyo kusababisha wenye vyombo vya moto kuchukua tahadhari kubwa ili kuepuka kupata madhara.
Hata hivyo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania( TMA) ilishatoa utabiri wa hali ya hewa kwa kueleza kutakuwa na mvua hasa leo Jumapili huku pia ikitoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari .
Aidha kwa nyakati tofauti viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini walishatoa maelekezo ya watu wanaoishi maeneo ya bondeni kuchukua tahadhari kwani TMA ilishatabiri uwepo wa mvua za Elnino.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...