Na Mwandishi Wetu
 
SHULE ya Msingi Hazina imeahidi kuendelea kuwa juu kitaaluma kwa kuhakikisha inakuwa na walimu mahiri na wenye wito wa kazi ya ualimu.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma wakati a mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Alisema shule hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhimiza elimu bora kwa kuwalea wanafunzi kimaadili na kuwapa ushauri unaowawezesha kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.
“Kwa kuzingatia kwamba dunia ya leo ni ya utandawazi ni jukumu letu kama walimu na walezi kuwaelimisha wanafunzi kuhusu kila wanachokifanya,” alisema

Alisema kwa miaka 17 tangu shule hiyo kuanzishwa imepata mafanikio makubwa kitaaluma kwani imekuwa na matokeo mazuri katika ngazi za wilaya, mkoa na hata kitaifa.

Alisema mwaka huu wameendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kuwa shule ya kwanza kiwilaya na katika mkoa wamefanikiwa kuingia kwenye kundi la kwanza la ufaulu (band 1) .

“Katika ngazi ya taifa wanafunzi wetu wote wamefanikiwa kufaulu huku shule yetu ikifanikiwa kupata daraja A la ufaulu katika mtihani wa taifa wa mwaka 2022 na kwa mwaka huu tunatarajia matokeo makubwa zaidi,” alisema

“Pia tumefanikiwa kuibua vipaji mbalimbali vya watoto kama mlivyoona kwenye maonyesho na hii ni dalili nzuri kwamba katika maisha yao ya baadae wataendelea vizuri sana,” alisema
 

Wanafunzi wa shule ya msingi Hazina wakiingia kwenye mahafali yao yaliyofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 

Wanafunzi wa shule ya msingi Hazina wakionyesha bunifu mbalimbali kwenye mahafali hayo
 

Wakionyesha ubunifu mbalimbali
 

Wahitimu wa shule ya awali na msingi Hazina wakiwa kwenye picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...