Na Mwandishi Wetu
SHULE zote nchini zilizonufaika na vifaa vya mradi wa Korean E-Learning Improvement Cooporation ( KLIC) ulio chini ya Ofisi ya Elimu ya Gwangju Metropolitan ya nchini Korea ya Kusini, wenye lengo la kuboresha elimu nchini katika eneo la TEHAMA, wametakiwa kutumia vizuri , kiusahihi na kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kunufaisha wanafunzi wengi zaidi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utafiti,Habari na Machapisho waTaasisi ya Elimu Tanzania(TET) Kwangu Masalu leo Novemba 8, 2023 katika shule ya Sekondari Kimbiji iliyopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam katika ziara ya ujumbe wa watu kutoka Korea ulipofika shuleni hapo
Lengo la kufika katika shule hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kugawa vifaa vya TEHAMA vya kujifunzia masomo na kutoa mafunzo ya vitendo ya namna ya kuvitumia kwa walimu na wanafunzi.
Mwakilishi wa walimu waliopo kwenye ziara hiyo kutoka nchini Korea Kusini, Kim Chi Gon ameeleza kuwa , wataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha wanakuza utumiaji wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.
Ameongeza kwa sasa ulimwengu umebadilika sana hasa katika eneo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kwa upande wa Kaimu Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kigamboni Twidike Ntima ameeleza kuwa shule hiyo kuwa moja ya shule za mfano wa kupata vifaa vya TEHAMA ni jambo kubwa ambapo imesaidia kwa walimu kufanya kazi kwa urahisi.
Amesisitiza kuwa na endapo masuala ya TEHAMA yataendelea kusambaa nchi nzima basi wanafunzi nchini na walimu wataweza kupiga hatua katika masuala ya elimu.
Awali Mkuu wa shule hiyo Joyce Ndaona amesema kwa sasa walimu wa shule hiyo wamepata mafunzo kutoka kwa wataalamu wa nchini Korea ya Kusini ambapo wamepata ujuzi wa kurahisishiwa kazi hasa katika eneo la ufundishaji na kuwapa nafuu wanafunzi kutumia TEHAMA kwenye ujifunzaji tofauti na awali.
Hata hivyo ugeni huo wa walimu na wanafunzi ukiwa katika shule hiyo ya Kimbjiji, uliweza kujionea namna wanafunzi wanavyoonesha uelewa katika masomo yao ambapo waliweza kuonesha utaalamu wao kupitia masomo ya fikizia na Uchoraji na baadae wanafunzi hao kuweza kufanya mafunzo kwa vitendo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...