-Ongezeko la matumizi holela ya Dawa za Antibiotiki

Na. WAF - Dodoma

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa mwilini (Antimicrobial resistance AMR) ni tishio kubwa la afya kwa jamii ya Watanzania hivyo Serikali imeweka mikakati madhubuti ili kukabiliana na tatizo hilo kwa kuimarisha udhibiti kwa kuondoa usimamizi wa maduka ya Dawa kutoka Baraza la Famasi na kupeleka majukumu haya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

Waziri Ummy amebainisha hayo kwenye ukurasa wake wa mtandao X wakati akijibu hoja ya Frank Arabi alipohoji kuhusu matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki.

Waziri Ummy amesema kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa nchini na hivyo kufanya dawa nyingi za Antibiotiki hivyo kuwa na ufanisi mdogo katika kutibu magonjwa.  

“Pamoja na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa za Antibiotiki, tatizo hii kwa kiasi kikubwa linachochewa na  baadhi ya wataalam wetu kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya taaluma”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amewataka wahudumu wa Afya hasa Madaktari na Wafamasia kusimamia jukumu hilo ili Watanzania wapate uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...