TIMU za soka na Netiboli za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA zimeanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA) yaliyoanza kutimua vumbi tarehe 12 Novemba 2023, Mkoani Dodoma.
Timu ya soka ya TPA imepata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro- NCAA, bao hilo pekee la ushindi limetiwa kimiani na
Ramadhani Madebe Katika dakika ya 15 ya mchezo.
Nayo Timu Bingwa ya mashindano haya kwa netiboli, Timu ya TPA wakiongozwa na Nyota wake mahiri Neema Mwahu,
imetoa kipigo kizito cha magoli 38 kwa 24 dhidi ya Timu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...