*DG ateuliwa kuwa mtendaji bora 2023

*Wakurugenzi wa Undeshaji, Fedha na TEHAMA, nao washinda

Na Mwandishi Wetu, Dar

Kwa mara ya pili mfululizo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba, ameibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la watendaji wakuu wa Taasis za Umma kwa mwaka 2023.

Mwaka jana, 2022  CPA. Kashimba alijishindia tuzo hiyo pia. Kwa kushinda tuzo kwa mwaka huu, inaonesha wazi kuwa Mkurugenzi  Mkuu huyo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) yupo makini katika utendaji wake.

Pamoja na CPA. Kashimba, wakurugenzi wengine wa PSSSF wameongoza katika makundi yao.

Wakurugenzi hao ni  Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi, ambaye ameshinda tuzo ya Mkurugenzi wa fedha wa mwaka,   Bw. Mbaruku Magawa, ambaye amekuwa mshindi wa tuzo ya Mkurugenzi Uendeshaji wa Mwaka na Bw. Gilbert Chawe, Mkurugenzi wa TEHAMA, ambaye yeye amekuwa miongoni mwa washindi wa tuzo ya Ubunifu na Teknolojia.

Tuzo hizo za umahiri wa uongozi zinazotambulika kama The Top 100 Executive List 2023 Awards zimetolewa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Akiongea katika tafrija ya kukabidhi tuzo hizo, Mgeni Maalum Thamsanqa Maqubela, kutoka  taasisi ya Global CEO Institute ya Jamhuri ya Afrika Kusini; aliwaasa vingozi waliokabidhiwa tuzo  kuendelea kuimarisha mbinu zao za kiuongozi ili kuleta tija na ufanisi.

Aidha aliwahakikishia kuwa Tanzania ina fursa nyingi za ukuaji wa haraka wa kiuchumi na kwa kuzingatia fursa za kibiashara zilizopo sasa Afrika; basi matarajio ni kuimarika kwa soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

Tuzo hizi zinaratibiwa na waratibu wa Top 100 Executive Tanzania na Global CEO Institute ya Jamhuri ya Afrika Kusini ili kutambua viongozi 100 mahiri kila mwaka kwa kutathmini utendaji, umahiri, ustadi, ubora na uwezo.

Tuzo hizi ni kielelezo cha umahiri na ukuaji wa taasisi katika kuonesha ukuaji wa faida, ukuaji kifedha, ubunifu na huduma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba (Kushoto), akipokea tuzo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza  "Tuzo za umahiri kwenye nyanja za uongozi kundi la Hifadhi ya Jamii (The top CEO of the year - Parastatals Category for year 2023), kutoka kwa mwakilishi wa Global CEO Institute ya Jamhuri ya Afrika Kusin Thamsanqa Maqubela, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini DSar es Salaa.

Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa (kushoto), akipokea tuzo ya “Mkurugenzi Uendeshaji wa Mwaka” wa Tuzo za Umahiri kwenye nyanja za uongozi kundi la Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Pastor Abraham Essuman, kutoka Ghana. Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa TEHAMA, PSSSF, Bw. Gilbert Chawe (kushoto), akipokea tuzo ya Ubunifu na Teknolojia katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri kwenye nyanja za uongozi kundi la Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Bw. Yunus Mwarabu, wa Ampola, Zanzibar. Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba (mwenye suti ya blue), akipongezwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Mbaruku Magawa (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Beatrice Musa-Lupi (kushoto) na Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kinondoni, Bi. Ritha Ngalo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba (wapili kushoto), akipongezwa na Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Gilbert Chawe (kulia),  Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Mbaruku Magawa (wakwanza kushoto) na Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kinondoni, Bi. Ritha Ngalo.
CPA. Kashimba (kushoto), akibadilishana mawazo na vingozi wenzake
Baadhi ya watumishi wa PSSSF.
CPA. Kashimba, akibadilishana mawazo na Mkurugezni Mtendaji wa ATCL, Bw.Ladislaus Matindi

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe (katikati) akifurahia ushindi huo na timu yake, Afisa Mkuu wa Uhusiano, Bi. Fatma Elhady (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi, Bi. Coleta Mnyamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...